Friday, March 2, 2018

Mbunge Jimbo la Nyamagana amfagilia Magufuli

Mhe Stanislaus Mabula hivi Leo ametembelea Kata ya Buhongwa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2015-2020 kupitia serikali ya awamu ya tano.

Ambapo amefanya Ziara maalumu shule mbili za msingi na kuhaahidi wananchi kuwa, ofisi yake kushirikiana na serikali wataezeka paa la  Vyumba vya madarasa shule ya msingi Buhongwa B kwa  madarasa Saba na shule ya Bulale  madarasa miwili kupitia Fedha za  " Local capital development grant" (LCDG).

Amewashukuru wananchi kushirikiana na halmashauri ya Jiji la  Mwanza kwa michakato yote ya kujitolea Kwa pamoja kuwezesha ujenzi huo kufanikiwa Kwa hatua iliyofikia.
Mheshimiwa mbunge amewaeleza wana nchi walio fulika katika mkutano huo ya kuwa hatuna budi kuendelea kumuombea afya na uhai mlefu,.

Rais wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayo endelea kuifanya ya kuwa jali wantanzania,
Mhe mbunge aliendelea kuwambia wananchi 
Hatuna budi kuendelea kumpongeza Rais wetu mpendwa na wasaidizi wake kwa namna wanavyo endelea kutujali wana nchi wa jimbo la  nyamagana .

Tumepata fedha kwa ajili ya kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji
Zaidi ya  ambayo ni sawa na shiringi  billions 112 zitatumika kujenga matenki ya maji  katika kata za ,Isamilo tenki lenye ujazo wa  lita million moja na  laki mbili (1200000).

kata ya pamba Bugarika na mahina  matenki mawili yenye ujazo wa lita million moja (1000000)
Mkolani tenki moja lenye ujazo wa lita million moja laki mbili(1200000) Ikiwemo kubadili mfumo wa mabomba ya zamani na kuweka mapya,.

Aliambatana na Katibu wa CCM wilaya, viongozi wa CCM Kata pamoja na baadhi ya watendaji wa Kata na  mitaa.
Imetolewa na,
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana

Tukutane Kazini





No comments:

Post a Comment