Mbunge Jimbo la Nyamagana kutatua kero ya ardhi kwa Kaya 636, kuboresha sekta ya elimu, afya na miundombinu na barabara pamoja upatikanaji wa Soko Kata ya Mahina.
Mhe Stanislaus Mabula akiongea na wananchi wa kata ya Mahina kuelezea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2015-2020.
Amesema uongozi wake umewezesha upatikanaji wa hati za viwanja vya makazi kwa Kaya 636 ambazo zitatolewa wiki mbili zijazo baada ya mchoro wake kukamilika na kunufaisha mitaa minne ya Kata hiyo.
Katika kuboresha sekta ya elimu mhe Mabula amewaambia wananchi amewezesha upatikanaji wa shilingi million 18,500,000 ambazo shilingi millioni 9,600,000 imeenda shule ya Nyaruguru kumalizia ujenzi wa darasa ambayo ina upungufu wa Vyumba vya madarasa 40. Kadharika shilingi 8,900,000 zimeenda katika ujenzi wa matundu ya vyoo bora shule ya sekondari ya Mahina ambayo ilikuwa imekwama.
Kukabiliana na changamoto ya Maji Safi na Usalama tayari serikali ya awamu ya tano imewezesha ujenzi wa matank mawili yenye uwezo wakuhifadhi Lita 1,000,000 tank mmoja linaweza kuhifadhi ujazo wa Lita 800,000 na lingine lita 200,000 na tayari mkandarasi anaendelea na Kazi.
Katika sekta ya afya amesimamia upatikanaji wa shilingi million 78,000,000 zitakazosaidia kukamilisha wodi la wanawake wajawazito na watoto ilikupandisha hadhi Zahanati hiyo kuwa kituo cha Afya.
Amefafanua serikali ya awamu ya tano imewezesha ujenzi wa barabara kutokea bendera tatu, Igeregele, Mahina shule ya msingi, Bugarika hadi kufika Bugando hospitali Kata ya Pamba ambayo iliwekewa jiwe la msingi na Mwenge wa Uhuru 2017. Ambapo Mwaka ujao wa Fedha barabara hiyo imitengewa Fedha kilometa 2 kwa kipande kilichobakia. Pia ujenzi wa barabara ya Mahina Kati, Tambukareli kutokea Kata ya Mkuyuni kupunguza msongamano wa Magari inatazamiwa kuanza.
Amemalizia kuipongeza ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza kwaushirikiano wake na Baraza la madiwani kutenga fidia ya shilingi millioni 60,000,000 kulipa eneo la Kiwanja kwaajili ya ujenzi wa Soko Kata hiyo.
Imetolewa na,
Ofisi ya mbunge,
Jimbo la Nyamagana







No comments:
Post a Comment