Halmashauri kutenga billion moja ya fidia, aelekeza uongozi wa BMU"Beach mangemant Unit" kuvunjwa Luchelele.
Mbunge Jimbo la Nyamagana amebainisha haya akiwa anandelea na ziara ya kuelezea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2015-2020 Kata ya Luchelele Ikiwa ni mwendelezo wa Ziara zake Kata zote 18 Za halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Mhe Mabula amewaambia wananchi amemwelekeza Afisa Uvuvi, mifugo na kilimo Jiji la Mwanza kuchunguza na kuvunja uongozi wa BMU "Beach management Unit" Swea eneo la Luchelele ambayo imekuwa inalalamikiwa na wananchi kwa ubadhilifu, tuhuma za rushwa, uvuvi haramu, kunyanyasa wananchi pamoja na uongozi kuwa madarakani kinyume na taratibu na kanuni zilizowekwa baada ya kupokea malalamiko ya wananchi..
Katika Mwaka huu wa Fedha halmashauri ya Jiji la Mwanza imetenga billion 1,000,000,000 kwaajili ya kulipia maeneo ya huduma za kijamii zikiwemo taasis za elimu na afya Kwa kata hiyo.
Alisema.
Mhe Mabula amebainisha uongozi wake umejipanga kukabiliana na changamoto ya miundombinu ya barabara Kwa kuendeleza mazungumzo na wadau wa Maendeleo ikiwemo taasis ya Poor Cleare ambayo imeafiki kujenga KM 2.5 za barabara kwa kiwango cha rami kutokea barabara kuu Mkolani inayoelekea Shinyanga kupitia shule ya wasichana Nyakahoja Nyahingi na kurahisisha ujenzi wa barabara ya Malimbe SAUT, Luchelele njia casamico kuelekea Ngaza kwa kiwango cha changalawe ili kuwezesha maeneo hayo na ya fukwe kufikika Kwa haraka na wepesi. .
Amebainisha serikali ipo katika hatua za mwisho kuanza urasimishaji wa maeneo Kata hiyo baada ya kukamilisha michoro ya hati za wananchi wa eneo ya mitaa Sita iliyokwisha pimwa ikiwemo mtaa wa Nyahingi.
Pia serikali imetenga Fedha kwaajili ya ujenzi wa wodi la Mama na mtoto pamoja na Wagonjwa wa kawaida Zahanati ya Shadi ilikuwezesha Kata hiyo kuwa na kituo cha Afya ambao ni Mpango wa serikali japo Kama Kata hiyo inazo Zahanati mbili..
Mwisho mhe mbunge alimshukuru Mhe Vicent Lutege Lusana diwani wa Kata hiyo, ofisi ya mkurugenzi pamoja na baraza la madiwani kwa umoja wao kuletea wananchi wa Kata hiyo Maendeleo.
Tulianza na Mungu
Tutamaliza na Mungu Ishara.
Imetolewa na,
Ofisi ya mbunge,
Jimbo la Nyamagana



No comments:
Post a Comment