Mazungumzo
kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Kampuni ya Bharti Airtel
inayomiliki hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania
yameanza rasmi leo tarehe 12 Machi, 2018 Jijini Dar es Salaam.
Katika
mazungumzo hayo kamati iliyoundwa na Mhe. Rais Magufuli inaongozwa na
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na timu ya Bharti
Airtel inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wake Bw. Mukesh Bhavnani.
Mazungumzo
hayo yanalengo la kufikia makubaliano yatakayokuwa na tija kwa pande
zote mbili (Serikali ya Tanzania na Bharti Airtel) na kuimarisha sekta
ya mawasiliano nchini Tanzania.
Kampuni
ya Bharti Airtel iliomba kufanyika kwa mazaungumzo hayo baada ya kamati
iliyofanya uchunguzi kuhusu umiliki wa kampuni ya Airtel Tanzania
kuwasilisha ripoti yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
12 Machi, 2018

No comments:
Post a Comment