Baadhi
ya wananchi wa Mtaa wa Nyakabale wilayani Geita wametelekeza mwili wa
marehemu nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa huu, Elias Ndarawa.
Ndarawa anatuhumiwa kutoshughulikia tukio la Zacharia Shaban kupigwa na polisi jamii hadi kufa.
Wananchi hao waliubeba mwili wa Zacharia na kuulaza kwenye kitanda cha mwenyekiti huyo.
Majaliwa
Shaban ambaye ni ndugu wa marehemu Zacharia amesema leo Machi 12,2018
kwamba nduguye alipigwa Machi 5,2018 akiwa eneo la Mgodi wa Dhahabu
Geita (GGM) akiokota mabaki ya mawe ya dhahabu maarufu magwangala.
Amesema Zacharia alipelekwa polisi alikokaa kwa siku sita na aliporudi uraiani hali yake ilikuwa mbaya.
Majaliwa
amesema nduguye alipelekwa hospitali alikofariki dunia Jumamosi Machi
10,2018 na hadi sasa hakuna kiongozi aliyefika kwenye msiba huo wala
kutoa kauli yoyote.
Mkazi
wa mtaa huo, Johnson John amesema hawapo tayari kuzika hadi Serikali
itakapotoa kauli kuhusu hatima ya maisha yao kwa kuwa polisi jamii
wamekuwa wakiwapiga na kuwajeruhi.
Jana,
Machi 11,2018 wananchi walivamia eneo la kituo cha polisi jamii
kilichopo mtaa wa Manga na kukichoma moto kwa madai kwamba wamempiga na
kumuua Zacharia

No comments:
Post a Comment