Spika Job Ndugai amefanya uteuzi wa wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Machi 12,2018 inasema Spika
amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Katibu ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Taarifa
hiyo imesema ibara hiyo imeweka wazi kwamba, Kanuni za Kudumu za Bunge
zinafafanua muundo wa shughuli za Kamati za Bunge.
“Kwa
msingi huo Kanuni ya 118 ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la
Januari, 2016 imeweka Kanuni za Kudumu za Bunge zenye muundo na majukumu
mbalimbali kama yanavyofafanuliwa katika nyongeza ya nane. Uteuzi wa
wabunge kwenye kamati mbalimbali unaonekana utaratibu katika Kanuni ya
116.”
“Kanuni
ya 116(1) inaweka utaratibu kwamba, ujumbe kwenye Kamati za Kudumu za
Bunge utadumu mpaka mwisho wa Mkutano wa Kumi wa Bunge ambao ni nusu ya
kwanza ya maisha ya Bunge,” anasema Spika Ndugai.
Katika
uteuzi huo, wajumbe mbalimbali wamerejea katika kamati zao, wengine
wakibadilishwa huku baadhi ya wenyeviti waliokuwa wakiongoza baadhi ya
kamati wameondolewa.
“Kwa
mamlaka niliyopewa na Kanuni ya 115(3) na kwa kuzingatia vigezo
vilivyoanishwa katika Kanuni ya 116(5) nimefanya uteuzi mpya wa ujumbe
katika Kamati za Kudumu za Bunge. Wajumbe wa kila kamati wanawajibika
kuchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwa mujibu wa Kanuni ya 116(10)
kuwa viongozi wao,” amesema

No comments:
Post a Comment