Monday, April 9, 2018

DIWANI KAWEKAMO AHITIMISHA ZIARA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI

Diwani wa kata ya Kawekamo Mhe Japhes Rwehummbiza amehitimisha ziara yake yenye lengo la kufafanua juu ya miradi ya maendeleo iliyotekelezwa ndani ya kata yake tangu kuchaguliwa kwa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Magufuli iliyojumuisha jumla ya matawi Matano ya Nyasaka ‘B’ , Pasiansi mashariki ‘B’ , Msumbiji, Nyasaka ‘A’ na Pasiansi mashariki ‘B’


 Akihitimisha ziara hiyo kwa Tawi la Nyasaka ‘A’  Mhe Japhes Rwehumbiza mbali na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Magufuli na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula kwa ushirikiano na msaada wao katika kufanikisha miradi mbalimbali ndani ya kata yake  ikiwemo mradi wa ujenzi wa daraja la Msumbiji, upanuzi wa barabara ya kutoka mjini kwenda uwanja wa ndege inayopita katika kata yake,  msaada wa madawati na vitabu kwa shule za kata yake kutoka ofisi ya mbunge, msaada wa milioni 2 kutoka taasisi ya HAKI elimu kuunga mkono jitihada za kuboresha elimu kwa shule ya Kilimani iliyopo ndani ya kata yake, kuendesha zoezi la urasimishaji wa makazi,  miradi ya maji safi na salama,  pamoja na kuelezea hatua alizochukua kusaidia miradi ya barabara za msumbiji, ppf kiseke na nyakurunduma kabla ya kuanzishw kwa wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA


‘… Ndugu wanachama kwanza nawashukuru kwa kujumuika pamoja siku ya leo ili tuweze kufahamishana kwa pamoja ni kipi tumetekeleza kwa kipindi hiki cha miaka miwili tangu mtuchague, Na kama mnavyojua kidole kimoja hakiwezi kuvunja chawa …’ Alisema


Aidha Mhe Japhes Rwehumbiza pia amewataka wananchi wa mtaa Nyasaka kuwa teyari kujitolea nguvu zao katika kufanikisha mradi wa ujenzi wa Zahanati itakayoanza kujengwa muda mfupi kutoka sasa baada ya kata yake kutengewa jumla ya milioni mia moja na teyari eneo limeshapatikana ili kufanikisha ujenzi huo utakaosaidia kuimarisha huduma za afya kwa wananchi 


Akifungua kikao hicho mwenyekiti wa Tawi la Nyasaka ‘A’ Comred Moshi Zoo mbali na kumpongeza diwani wa kata hiyo na mbunge wake kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya mtaa wake amewahakikishia ushirikiano viongozi hao ili kuendelea kujiletea maendeleo huku katibu wa Itikadi na Uenezi Comred Paul Mitenga akiwataka wanachama wa CCM kuwa wamoja na kuacha makundi sambamba na kumshukuru diwani kwa kutoa kadi Tisini za chama cha mapinduzi na jumuiya zake kama jitihada za kuongeza wananchama na kukiimarisha chama hicho


Kikao hicho pia kilihudhuriwa na wataalamu wa Serikali kutoka ofisi ya mtendaji wa kata ya Kawekamo pamoja na viongozi wa chama kutoka kata waliohamasisha wanachama kuhakikisha wanairudisha katika utawala wa CCM mitaa yote iliyopo upinzani ya ndani ya kata hiyo


' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '




No comments:

Post a Comment