Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula ametumia fursa hiyo pia kumshukuru aliyekuwa katibu wake Comrade Kheri James ambae sasa ni Mwenyekiti wa UVCCM (T) kwa ushirkikiano mkubwa aliyompa katika utekelezaji wa Ilani Jimboni, Aidha aliwashukuru waratibu wa ofisi ya mbunge ngazi ya kanda kwa maana ya kanda ya Bugogwa, Kirumba, Nyakato na Ofisi kuu kwa ushirikiano wao mkubwa uliowezesha mambo yote kwenda sawia.
Taarifa ya utekelezaji wa Ilani
inawasilishwa kwa kuzingatia katiba ya CCM Ibara ya 73 (3) na Ilani ya uchaguzi
Ibara 180 taarifa hiyo yenye kurasa 88 imeainisha mambo mbalimbali kulingana na
Sekta .
Ambapo Mhe Dkt Mabula aliainisha
utekelezaji huo kwa namna ambavyo Serikali kuu, Halmashauri, Mfuko wa Jimbo na
Taasisi ya The Angeline Foundation kwa kushirikiana na Wadau walivyowezesha
utekelezaji huo kuanza na Mfuko wa Jimbo Shilingi 106,685,600 zimetumika
kutengeneza madawati 530, Shilingi 53,156,600 kuchonga barabara mpya yenye Km
27.6, Shilingi 44,500,000 kujenga Kivuko kata ya Mecco, Shilingi 4,000,000 na
Ujenzi wa Kivuli cha kituo cha afya Kirumba Shilingi 5,029,000.
Huku Jumla ya shilingi 12,300,000
zikitumika katika kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa mabalozi 1403 walipatiwa
elimu hiyo na wanachama wapatao 3756 wamefundishwa ambapo Mhe Dkt
Angeline Mabula alizishukuru taasisi za Intergrity Foundation na
Sudama Investment kwa kuwezesha mafunzo ya wajasiriamali wakishirikiana na
taasisi ya The Angeline Foundation
Upande wa sekta ya Ardhi jumla ya viwanja
15564 vimepimwa kupitia upimaji shirikishi kufikia Desemba 2017 na hati 5502
zilikuwa zimetolewa, Aidha kati ya migogoro ya ardhi yote iliyomfikia mbunge
huyo, amesema asilimia 90 ya migogoro hiyo imetatuliwa na kuahidi changamoto
iliyopo katika mgogoro wa airport na wananchi wa Shibula utapatiwa ufumbuzi
muda si mrefu alisema Dkt Mabula
Sekta ya Miundombinu , Fedha toka Serikali
kuu shilingi 500,000,000 zimetumika katika kituo cha fya Karume kujenga
miundombinu yote muhimu, Huku shilingi 1,200,000,000 zikitumika kukarabati
miundombinu ya barabara na madaraja fedha toka mfuko wa barabara, na kwa sasa
kuna miradi 14 ya ujenzi wa barabara ambapo wakandarasi wako site na katika
hatua nyengine Dtk Mabula alifanya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya
Kitangiri mzunguko-Kabuhoro Ziwani yenye Km 3 ambapo Km 1.5 ya barabara
hiyo inajengwa na GeminiContractors Ltd ambapo Dkt Mabula alitoa shukrani kwa
Mhe Dkt John Magufuli kwa hatua nzuri ya upanuzi wa Uwanja wa ndege, Ujenzi wa
daraja la Furahisha na kutengewa fedha Bilioni 2.3 kwaajili ya ujenzi wa Kivuko
cha Kisiwa cha Bezi na Kayenze.
Ili kuendana na teknolojia ya kisasa,
Jumla ya kompyuta 11 zilipokelewa na kupelekwa katika vituo 3 vya afya na
zahanati 7 na Kompyuta nyengine 60 zilipelekwa shule ya sekondari za
Buswelu kompyuta 20, Bwiru kompyuta 20 na Bugogwa kompyuta 20, Aidha
madawati 28 yamejengwa 22 tayari na kukamilika na madarasa 6 yakiendelea
kujengwa
Pamoja na hayo Mfuko wa Angeline
Foundation umetumia shilingi 265,418,800 katika shughuli za mafunzo ya
ujasiriamali, Shilingi 12,300,000 utengenezaji barabara, 13,717,000 madawati 1923,
Shilingi 163,455,000.
Sekta ya Elimu, Sera ya Elimu bure
imefanya uandikishaji darasa la kwanza kuongezeka hadi kufikia 113%, Jumla ya
shilingi 3,428,819,376 zilipokelewa katika shule zetu kwajili ya gharama za
utawala katka shule zote jimboni, Ukarabati wa shule Kongwe shilingi
825,841,642 zilizopokelewa kukarabati shule ya sekondari Bwiru wavulana
madarasa 19, mabweni 11, jengo la utawala, maabara 2, maktaba 1, vyoo 9 na
mfumo wa maji na umeme
Upande wa Michezo jumla ya shilingi
17,950,000 zimetumika katika kuimarisha michezo kuanzia ngazi ya shule za
msingi, sekondari na mashindano ya Jimbo Cup
Upande wa miradi ya maji mikubwa
imetekelezwa chini ya ufadhili wa benki ya uwekezaji ya Ulaya Euro 104.5
milioni na Euro 14.7 milioni kutoka shilika la maendeleo la ufaransa,
Miradi ambayo ikikamilika itatoa suluhu ya tatizo la maji jimboni sambamba na
uchimaji wa visima 10 inaendelea vyema katika maeneo ya vijijini
Upande wa kuimarisha chama jumla ya
shilingi … zilitumika kununua tairi za gari la chama, kuchangia mikutano ya
chama na jumuiya zake na kuchangia ujenzi wa ofisi ya chama
Katika suala zima la uwezeshaji wananchi
kiuchumi Halmashauri ya manispaa ya Ilemela imetumia Shilingi 283,000,000
kwaajili ya wanawake na vijana jumla ya vikundi 129 vimenufaika wanawake
vikundi 82 na vijana vikundi 47 huku akiwaasa wananchi na viongozi kuendelea
kushirikiana katika kuwaletea wananchi maendeleo
'... Ndugu zangu kwanza
nawashukuru kwa kukipa ridhaa chama cha mapinduzi kuweza kushika dola, na mimi
muwakilishi wenu kama inavyonitaka katiba ya chama cha mapinduzi ibara ya 73 na
Ilani ya uchaguzi ibara ya 180 nina wajibu wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa
ilani kwa kipindi hiki cha miaka miwili ili mpate kujua
tumewafanyia nini kwa kushirikiana na Serikali na Viongozi wenzangu kwa maana
ya mheshimiwa Rais, mbunge na madiwani ...' Alisema
Akifungua mkutano huo mwenyekiti wa ccm
wilaya ya Ilemela Nelson Meshack amewaambia wananchi
waliohudhuria mkutano huo kuwa mkutano mkuu wa utekelezaji wa Ilani ni mkutano
halali na wa kikatiba wenye lengo la kuwapa wanachama na wananchi fursa
ya kujua serikali waliyoichagua na viongozi wao wamewafanyia kitu gani katika
kuwaletea maendeleo
Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu
ya chama cha mapinduzi kupitia kundi la wabunge Mhe Lusinde amewataka viongozi
na wanachama wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ilemela kuwa na moyo wa kuthamini
mchango wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo unaofanywa na viongozi
waliowachagua na kuwa mstari wa mbele kwa kuyasema mazuri yanayofanywa na
Serikali ya chama cha mapinduzi na viongozi wake huku akikemea vitendo vya
usaliti, majungu na utumiaji vibaya wa mamlaka kwa kuwagawa wanachama
Akihitimisha mwenyekiti wa umoja wa vijana
wa chama cha mapinduzi Kheri James amekemea vitendo vya baadhi
ya wanachama na viongozi vya kukwamisha utekelezaji wa Ilani katika kuwaletea
wananchi maendeleo na kuongeza kuwa chama cha mapinduzi hakitamvumilia mtu
yeyote atakae kwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa maslahi yake
binafsi sambamba na kuwaasa kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Mhe John
Magufuli na Mbunge Dkt Angeline Mabula kwa jitihada zao za kuwaletea wananchi
maendeleo
Mkutano mkuu huo maalum pia ulihudhuriwa
na watumishi wa umma wa Jimbo la Ilemela, taasisi za umma, mashirika binafsi,
na viongozi mbalimbali wa maeneo mengine wakiongozwa na katibu wa CCM mkoa
Mwanza
' Ilemela ni yetu, tushirikiane
kuijenga'
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
10.04.2018







No comments:
Post a Comment