Mashindano ya Ilemela Jimbo Cup yataendelea kuibua vipaji vipya vya michezo pamoja na kuendeleza vipaji vya zamani
Kauli hiyo imetolewa na katibu wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula, Comred Michael Goyele wakati wa fainali za mashindano ya kusaka timu ya kata itakayowakilisha kata ya Kitangiri katika mashindano ya Ilemela Jimbo Cup 2018 yaliyofanyika kata ya Kitangiri na kuhusisha Timu ya TP Mazembe kutoka tawi la Mihana dhidi ya timu ya Jiwe Kuu Fc kutoka tawi la Jiwe kuu ambapo amewahakikishia kuwa mbunge wao ana dhamira njema ya kuendeleza michezo jimboni humo kupitia mashindano ya jimbo cup kama sehemu ya kuibua vipaji vipya pamoja na kuendeleza vile vya zamani
' mheshimiwa mbunge ana dhamira njema dhidi yenu, malengo yake ni kuona vijana wa jimbo lake wananufaika kupitia vipaji vyao, Sasa kupitia mashindano haya ya kata tunategemea kupata timu nzuri itakayoshiriki mashindano ya jimbo cup ...' Alisema
Aidha katibu huyo wa ofisi ya mbunge amesisitiza kuwa ofisi ya mbunge itaendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali katika kuhakikisha zinatoa fursa kwa vijana kutumia vipaji vyao kuweza kujikwamua kiuchumi pamoja na kuimarisha afya zao
Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi kata Kitangiri, Comred Katema mbali na kumshukuru mwakilishi huyo wa mbunge kwa kujumuika pamoja katika fainali hizo amempongeza kwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa ili kuendeleza vipaji vya vijana wa jimbo hilo pamoja na kuwaasa vijana wa kata hiyo kuwa na nidhamu na kuendeleza umoja katika kufikia ndoto zao
Fainali hizo ziliisha kwa timu ya Jiwe kuu kucharazwa goli mbili dhidi ya TP Mazembe kisha kuondoka na mbuzi wawili dhidi ya mbuzi mmoja aliyechukuliwa na timu ya Jiwe kuu kama mshindi wa pili huku mshindi wa tatu akiambulia mpira mmoja na mchezaji bora akipata jezi moja kama zawadi kupitia mashindano hayo
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
24.04.2018
No comments:
Post a Comment