Rais
Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Bodi ya National Microfinance Bank
(NMB) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo kuangali kiasi cha
gawiwo kinachotolewa na benki hiyo, kutokana na kiasi hicho kutoongeza
ndani ya miaka mitatu mfululizo.
Rais
Magufuli ameyasema hayo jana Mjini Dodoma wakati alipokuwa akifungua
jengo jipya la Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF) pamoja na
tawi jipya la NMB Kambarage lililoko katika jengo hilo.
“Kuna
mambo mazuri mengi yaliyofanywa na NMB lakini tunahitaji uhakiki wa
gawiwo linalotolewa kwa Serikali, kutokana na gawiwo hilo kutopanda kwa
miaka mitatu mfululizo tangu mwaka 2014/2015 mpaka mwaka 2016/2017
ambapo benki hiyo imekuwa ikitoa shilingi Bilioni 16.525 kama gawiwo la
hisa ya asilimia 32 iliyonayo katika Benki hiyo,” alisema Rais Magufuli.
Ameendelea
kwa kusema, ni matumaini yake kuwa kiasi hicho cha fedha kitapanda kwa
mwaka 2017/2018 kutokana na benki hiyo kutengeneza faida kila mwaka.
Aidha,
Rais Magufuli ameipongeza benki ya NMB kwa kuwa na matawi mpaka
vijijini pamoja na kutoa ajira kwa zaidi ya Watanzania 3000 na kutoa
misaada ya kijamii ikiwemo madawati 600, kompyuta 300 kwa shule za
Sekondari na vitanda vya wagonjwa.
Vilevile
Rais Magufuli ameupongeza mfuko wa PSPF kwa kuona fursa ya Serikali
kuhamia Dodoma na kujenga jengo ambalo limeboresha na kupendezesha
mandhari ya Dodoma ambapo pia ujenzi huo umetoa ajira kwa Watanzania
takribani 250.
Pia
amesema, mfuko huo umekuwa ukitoa mikopo kwa wanachama wake pamoja na
kuwekeza katika ujenzi wa viwanda mbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwanda
cha cha Sukari Kagera, kiwanda cha nguo na turubai vilivyopo mkoani
Morogoro.
Wakati
huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema Rais
Magufuli kupitia TAMISEMI ametoa shilingi bilioni 70 kwa ajili ya ujenzi
mbalimbali wa miundombinu mkoani Dodoma.
Dkt.
Mahenge ametaja miundombinu hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa stendi
mpya ya kisasa yenye uwezo wa kuingia mabasi makubwa 250, magari madogo
600 pamoja na bajaji na bodaboda 300 kwa wakati mmoja.
Aidha,
Dkt Mahenge ameitaja miundombinu mingine ambayo ni ujenzi wa soko la
kisasa, sehemu ya kupaki malori, miundombinu ya majitaka, maeneo ya
kupumzikia pamoja na kuboresha miundombinu ili kuondoa msongamano wa
magari.
kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji
ameutaja mfuko wa PSPF kuwa ndio mfuko wa kwanza kuwekeza katika vitega
uchumi Makao Makuu ya Nchi ukiondoa mfuko wa LAPF ambao Makao Makuu yake
yapo Mkoani Dodoma.
Jengo
la PSPF ni moja ya majengo marefu yaliyoko mkoani Dodoma ambapo ina
jumla ya ghorofa 11 pamoja na eneo la maegesho ya magari 161 ambapo
mpaka sasa jengo hilo limeshapata wapangaji kwa asilimia 100.
No comments:
Post a Comment