Aliyekuwa
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ameushangaza umma baada ya kuwepo na
taarifa za kutarajia kuoa mke wa tano, binti mdogo mwenye umri wa miaka
24.
Taarifa
hizo zimethibitishwa na binti huyo ambaye ni mke mtarajiwa wa Zuma
anayejulikana kwa jina la Nonkanyinso Conco, kupitia chombo cha habari
cha Times live cha nchini Afrika Kusini.
“Ndio
tunaoana, hayo ndiyo naweza kusema kwa sasa, nahitaji kutoa taarifa
kabla sijafanya interview (mahojiano) yoyote”, amesikika binti huyo
akiuambia mtandao wa Times Live.
Habari
zaidi zinasema kuwa binti huyo tayari ana mtoto mchanga aliyezaa na
Jacob Zuma ambaye amezaliwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Jacob
Zuma, April 12, na tayari mahali imeshatolewa.
Jacob Zuma ambaye ana miaka 76 mpaka sasa ameshaoa mara sita, na hii itakuwa ni mara ya saba kufunga ndoa,
Tukio
hilo limeonekana kuwakwaza wananchi wa Afrika Kusini na kutoa maoni yao
kwenye mitandao ya kijamii, wakisema binti huyo ni mdogo sana kwa Zuma,
kwani wana tofauti ya miaka 52.
No comments:
Post a Comment