WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mkuu wa Mkoa Mstaafu,
Bw. Abbas Kandoro ambaye amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa
mjini Dodoma akipatiwa matibabu.
Akiwa
hospitalini hapo jana (Jumatano, Aprili 25, 2018), Waziri Mkuu
amefarijika baada ya kumkuta Bw. Kandoro na wagonjwa wengine waliolazwa
kwenye hospitali hiyo wakihudumiwa vizuri.
Pia
Waziri Mkuu amemjulia hali Mbunge wa Viti Malumu (CUF) Bi. Shamsiha
Azizi Mtambo ambaye amelazwa katika ya Wodi ya Uangalizi Maalumu
(ICU)kwenye hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu.
Waziri
Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa hao na kuwaeleza kwamba
madaktari wataendelea kuwahudumia vizuri ili kuhakikishia afya zao
zinaimarika na kurejea katika shughuli zao za kila siku.
Kwa
upande wake, Bw. Kandoro alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake
na kwenda kumjulia hali, pia aliwashukuru madaktari na wauguzi wa
hospitali hiyokwa huduma nzuri wanazompatia tangu alipofika hospitalini
hapo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
No comments:
Post a Comment