Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma
salamu za pole kwa familia ya Agness Gerald Waya kufuatia kifo cha mtoto
wao Agness alimaarufu kama Masogange kilichotokea Ijumaa.
Rais
Magufuli ametuma salamu hizo kupitia kwa Mwenyekiti Jumuiya ya Umoja wa
Vijana UVCCM Bw. Kheri James na kusema kuwa amesikitishwa sana na kifo
cha binti huyo kwani kifo chake kinapunguza idadi ya vijana ambao ndiyo
jeshi na watu ambao wanaweza kufikisha mbali taifa.
"Kupitia
jukwaa hili naomba nitoa salamu za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ambaye leo amewasili mjini Dodoma lakini ameomba niwasilishe
kwenu salamu za pole kwa kuondokewa na kijana mwenzetu,
"Mwenyekiti
anafahamu nchii hii sisi vijana ndiyo warithi wa taifa hili sisi ndiyo
tumebeba dira ya kulifikisha taifa ambapo tunadhani linafaa kufika hivyo
anasikitishwa sana kuona katika jeshi kubwa kama hili la vijana
tunapungukiwa na vijana wenzetu wanaondoka na kupunguza idadi ya askari
wetu , naomba mpokee salamu za Mwenyekiti wetu" alisema Kheri James
No comments:
Post a Comment