Rais
John Magufuli ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wakurugenzi wanaowanyima
haki zao wafanyakazi kwa kuwahamisha bila kuwalipa posho ya uhamisho.
Ameyasema
hayo mkoani Iringa leo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya
Wafanyakazi duniani, ambayo kitaifa yamefanuika mkoani humo.
“Ukimuhamisha
mtumishi mlipe fedha yake kabla ya kumuondoa na hili nalisema kwa mara
ya mwisho sitarudia tena kulizungumza hilo katika maisha yangu.
“Leo
nimeona bango jingine nafikiri chama cha walimu kinachosema wao
wanaendelea kuhamishwa bila kulipwa fedha za uhamisho, najua viongozi
wanaosimamia wizara zinazohamisha wako hapa, kama kuna mtu yeyote
anahamisha bila kulipa huyo ni jeuri na dawa yake ni kumtoa”, amesema
Rais Magufuli.
Pamoja
na mambo mengine, Rais Magufuli amewataka wananchi wa Iringa na Njombe
kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Ukimwi kutokana na mikoa hiyo
miwili kuongoza kwa ugonjwa huo nchini.

No comments:
Post a Comment