Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limemuomba Rais John Magufuli
kuangalia namna ya kuongeza mshahara wa kima cha chini angalau kisiwe
chini ya Sh250, 000.
Hayo
yamesemwa leo Mei Mosi na Katibu Mkuu wa Tucta, Dk Yahaya Msigwa wakati
wa sherehe za wafanyakazi, zinazoadhimishwa kitaifa katika viwanja vya
Samora mkoani Iringa, ambapo Mgeni Rasmi ni Rais John Magufuli.
Amesema
maisha kwa walio wengi yanakuwa magumu kutokana na kupanda kwa bei za
vitu muhimu ikiwemo vyakula na huduma za msingi za maisha.
“Tunaomba
Rais wetu kima cha chini kisipungue 250,000 kwa mwezi , lakini pia
tunaiomba Serikali kubuni vyanzo vingine vya mapato ili kuongeza wigo wa
utoaji huduma kwa watumishi au wafanyakazi, kuna mfanyakazi anapata
Sh100,000 hii haitoshi kitu kwa mtu mwenye familia yenye watoto wanne,”
amesema Dk Msigwa.
Aidha
alitoa wito kwa Serikali kuangalia upya namna ya kubuni vyanzo vingine
vya mapato ili kupunguza machungu kwa wafanyakazi kwani wanakatwa kodi
kubwa.

No comments:
Post a Comment