Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Balozi Augustino Maiga amefunguka na kumuomba radhi Rais Dkt. John
Pombe Magufuli kwa niaba ya watu wa Iringa kwa kukosa kura 25 za
udhamini katika kipindi cha kampeni za uchaguzi 2015.
Balozi
Maiga amesema hayo leo Mei 1, 2018 kwenye maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi duniani ambayo kitaifa inafanyika katika uwanja wa Samora
mkoani Iringa ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Kuunganishwa kwa mifuko
ya hifadhi ya jamii kulenge kuboresha mafao ya wafanyakazi"
"Nakumbuka
Mhe. Rais ulipata shida kidogo kupata wadhamini hapa Iringa Mjini
ikabidi utoke nje ya mji ndiyo ukapata, ila wadhamini 25 kwa hapa mjini
kura hazikupatikana tunakuomba radhi sana Mhe. Rais kwa kukosa busara
hiyo lakini ulipokuwa hapa ulitoa ahadi kwa wana Iringa na umezitimiza,
ahadi ya kwanza ulisema Iringa itakuwa Makao Makuu ya Utalii ya mikoa ya
kusini hilo tumeshalifanya, Mkuu wa mkoa aliitisha vikao na watu wa
mikoa mingine lakini hasa wewe umeshafanya maamuzi kuwa Uwanja wa ndege
wa Iringa wa Nduli utarekebishwa na kuweza kuchukua ndege kubwa zaidi
kama zile za Bombidier"
Aidha Maiga aliendelea kusema kuwa
"Na
umeshachukua maamuzi kwamba barabara ya kutoka hapa Iringa kwenda
hifadhi ya Ruaha itakuwa katika kiwango cha lami mara nyingi na mimi
nimekuwa nakuomba na kukukumbusha kuhusu maendeleo ya mkoa wa Iringa,
umenisikiliza na kutekeleza hapa Iringa pekee yake mjini barabara
zimetengenezwa kwa kutumia bilioni 6.4, shule kongwe kwama vile
Tosamaganga, Malangali zimeboreshwa, miradi ya afya na maji ni mabilioni
siwezi kusema lakini kubwa kabla ya kufika hapa umefungua barabara kuu
ya Afrika ya Kati na Afrika Mashariki, barabara hii inapita katikati ya
mkoa wa Iringa juzi pale Isimani umesema barabara hii iwe mkombozi kwa
watu wa Iringa"

No comments:
Post a Comment