Rais
Donald Trump amesema mkutano wake na kiongozi wa Korea Kim Jong Un
uliopangwa kufanyika Juni 12 huko Singapore hautafanyika.
“Nilikuwa na subiri kwa hamu kuwa pamoja na wewe,” Trump amesema katika barua aliyo muandikia Kim iliyotolewa na White House.
Barua
hiyo imeeleza pia kuwa: “Kwa masikitiko, kutokana na kuonyesha hasira
na uchokozi ulio wazi katika matamko yako ya hivi karibuni, nina hisi
haistahili kwa wakati huu kuwa na mkutano huu uliopangwa muda mrefu.”
"Unazungumzia uwezo wako wa nyuklia, lakini wetu ni mkubwa na wenye nguvu kiasi kwamba namuomba Mungu zisitumike kabisa" aliongeza.
"Unazungumzia uwezo wako wa nyuklia, lakini wetu ni mkubwa na wenye nguvu kiasi kwamba namuomba Mungu zisitumike kabisa" aliongeza.
Kitu
cha mwisho kilichoharibu mazungumzo haya, kwa mujibu wa afisa wa White
House, ilikuwa ni tusi dhidi ya Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence
mapema Alhamisi katika tamko la waziri wa mambo ya nje wa Korea
Kaskazini, Choe Son Hui.
Mwanamke
huyo alimwita Pence “ni karagosi la kisiasa” na kuonya kwa tamko la
kisiasa kauli inayofanana na matamko ya Pyongyang ya malumbano juu ya
silaha za nyuklia.
No comments:
Post a Comment