Bajeti
Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 ambayo ni ya tatu kwa
Serikali ya Rais John Magufuli, itasomwa na Waziri wa Fedha na Mipango,
Dk Philip Mpango kesho Alhamisi.
Spika
wa Bunge, Job Ndugai amesema "Juni 16 Waziri wa Fedha na Mipango
atasoma Bajeti Kuu ya serikali. Baada ya hotuba hiyo ya Waziri wa Fedha
tumewaandalia futari wageni wote waalikwa. Siku hiyo tutakuwa na wageni
wengi wa serikali."
Ndugai alisisitiza kwamba wabunge wote wawepo siku hiyo, wakati bajeti itakaposomwa.
Alisema
anajua bado kuna hati hati, kuwa huenda sikukuu ya Idd itakuwa Ijumaa,
lakini jambo muhimu wabunge wawepo siku ya Alhamisi kwenye hotuba ya
bajeti na kisha kwenye futari pamoja na wageni waalikwa.
Alieleza
kuwa baada ya hotuba hiyo, kusomwa bungeni ndipo wabunge wanaweza
kwenda kuungana na familia na ndugu zao, kusherehekea sikukuu hiyo
kubwa, inayoashiria kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akiwasilisha
Mapendekezo ya Serikali ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/19 kwa
wabunge Machi 13, mwaka huu mjini Dodoma, Dk Mpango alieleza kuwa katika
bajeti hiyo Serikali inatarajia kukusanya na kutumia Sh trilioni
32.476, ikiwa ni ongezeko la Sh bilioni 764 ukilinganisha na bajeti ya
mwaka 2017/18.
Mpango
alitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kuwa ni mradi wa Kituo cha Kuzalisha
Umeme cha Stiegler’s Gorge katika Mto Rufiji kitakachozalisha megawati
2,100, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro
kilometa 300 na Morogoro hadi Makutupora kilometa 336 na uboreshaji wa
Shirika na Ndege Tanzania (TTCL).
Pia,
ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi
Tanga, uzalishaji wa makaa ya mawe na umeme Mchuchuma na Liganga,
uendeshaji wa shamba la miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari Mkulazi
mkoani Morogoro na uboreshaji wa bandari za Tanga, Dar es Salaam na
Mtwara.

No comments:
Post a Comment