Mbunge
wa Kibakwe (CCM) George Simbachawene amewasilisha azimio la kuitaka
Serikali kuharakisha mchakato wa Muswada wa Sheria ya kuifanya Dodoma
kuwa makao makuu na kuuleta bungeni.
Akiwasilisha
azimio la kumpongeza Rais John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuendeleza
mji wa Dodoma na kuupa hadhi ya jiji, leo Juni 12 bungeni, Simbachawene
amesema ikiwezekana Muswada huo usomwe mara ya kwanza katika mkutano wa
11 unaoendelea.
"Naiomba
Serikali kuongeza raslimali fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu
mbalimbali itakayoendana na hadhi ya makao makuu na jiji kama vile
ujenzi wa Barabara zenye kiwango, miundombinu ya majisafi na majitaka,
upimaji na upangaji mzuri wa jiji la Dodoma," amesema.
Simbachawene
pia ameliomba Bunge kumpongeza kwa dhati Rais Magufuli na kumuunga
mkono kwa uamuzi wake wa kuifanya Dodoma kuwa jiji na hivyo kuliandaa
jiji la Dodoma kuendana na hadhi ya Makao Makuu ya Serikali.

No comments:
Post a Comment