Serikali
kupitia Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 imepanga kutumia shilingi 22.5
kwaajili ya matumizi ya uzazi wa mpango.
Akizungumza
leo, Juni 13, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, Waziri wa Wizara hiyo, Ummy
Mwalimu amesema kutoka katika vyanzo vya ndani kiwango hiki ni sawa na
ongezeko la asilimia 60 kutoka mwaka 2017/2018.
“Kwa
mwaka wa fedha 2018/2019 serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi
Bilioni 22.5 kwaajili ya uzazi wa mpango kutoka katika vyanzo vya ndani
kiwango hiki ni cha fedha sawa na ongezeko la asilimia 60 kutoka mwaka
2017/2018,” amesema Ummy.
Hayo
yameelezwa baada ya Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi kuihoji
serikali kuwa “Mahitaji halisi ya fedha kwaajili ya uzazi wa mpango kwa
mwaka kwasasa ni zaidi ya Sh. Bilioni 36 , Je, Serikali ina mpango gani
wa kutenga fedha zaidi ili kufikia kiasi kinachohitajika kwaajili ya
wakina mama na watoto?”

No comments:
Post a Comment