Serikali imatoa ajira kwa watumishi
2,160 katika shule za sekondari nchini ambapo kati yao waalimu 1900 ni
wa masomo ya sayansi na hisabati.
Akizungumza leo jumatatu Agosti
20,2018 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amesema
kati ya watumishi hao walioajiriwa 100 ni waalimu wa lugha na 160 ni
fundi sanifu maabara.
Amesema watumishi hao wanatakiwa kuripoti
katika ofisi za wakurugenzi wa halmashauri zilipo shule walizopangiwa
kuanzia Agosti 23,2018 hadi Septemba 5,2018.
“Watumishi hao
wanatakiwa kuripoti kwa muda huo wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya
kidato cha nne na kidato cha sita, vyeti halisi vya kitaalam vya mafunzo
ya ualimu vya ngazi husika pamoja na cheti cha kuzaliwa, na hatimaye
kwenye shule walizopangiwa” amesema Jafo.
Hata hivyo, Jafo
amewataka waajiriwa hao kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi na si makao
makuu ya halmashauri ili kuomba kuhamishiwa vituo vya kazi.
“Mwajiri
yeyote atakayechukua posho ya kujikimu kisha asiripoti kwenye kito
chake cha kazi serikali itamchukulia hatua za kinidhamu,” amesema Jafo
Jafo
ametumia nafasi hiyo kuwataka wakurugenzi wa halmashauri zenye vituo
vya kazi walizopangiwa watumishi hao kuwapokea na kwa kufuata taratibu
zote na kanuni za utumishi.
No comments:
Post a Comment