Thursday, September 20, 2018

M/KITI UVCCM TAIFA NDUGU KHERI DENIS JAMES AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MISUNGWI.

M/Kiti UVCCM Taifa  Ndugu Kheri Denis James leo hii amekagua miradi ya maendeleo  katika wilaya ya Misungwi. Akizungumza na vikundi mbalimbali amewapongeza sana viongozi wa serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuendelea kutekeleza Ilaniya Chama cha Mapinduzi.

 Pia Amewaasa vijana wanaonufaika na Miradi ya Serikali kuhakikisha wanajituma ili waweza kutimiza malengo yao. Aidha amewaambia vijana wote kuwa HAKUNA SHORTCUT inatakiwa wajitume.

Baada ya kukagua Miradi ya maendeleo M/Kiti wa Taifa Ndugu Kheri Denis James alipata nafasi ya kuongea na wanachama wa wilaya ya Misungwi ambapo katika hotuba yake amewaasa wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuwa na Umoja, Mahusiano Mazuri baina ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Viongozi wa Serikali na Wanachama kwa Ujumla .

Pia amewaasa vijana wa Misungwi na watanzania kwa Ujumla kuwa Serikali imetenga hela kwa ajili ya vijana ni swala la vijana kuwatayari kufanya kazi.















No comments:

Post a Comment