Sunday, September 9, 2018

SHIBULA YATINGA NUSU FAINALI ANGELINE JIMBO CUP 2018.

Timu ya Kata ya Shibula imefanikiwa kutinga nusu fainali katika mashindano ya mpira wa miguu ya Angeline Jimbo Cup 2018 mara baada ya kuifunga Timu ya Kata ya Mecco magoli 2-0 mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Jeshini Iyale.

Akizungumza mara baada ya kuisha kwa mchezo huo, Nahodha wa Timu ya Kata ya Shibula Ndugu Emanuel Lubala amesema kuwa matokeo walioyapata yametokana na kujipanga vizuri na kufanya mazoezi yakutosha sambamba na kuwahakikishia mashabiki wa Timu yake kuwa Timu hiyo itazidi kufanya vizuri kwa mechi zijazo

‘… Mchezo wa leo ulikuwa mzuri na tulijipanga lakini sababu kubwa iliyotufanya tufanye vizuri ni mazoezi yakutosha hivyo nawahakikishia tutaendelea kufanya vizuri na Timu zote tutakazo kutana nazo zijiandae kwa kipigo …’ Alisema

Nae Katibu wa UVCCM kata ya Mecco Ndugu Gasper Mwinyimvua mbali na kumshukuru mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kuanzisha mashindano hayo yanayotoa fursa kwa vijana wa kata yake kuonesha vipaji walivyonavyo, amewataka mashabiki wa Timu ya kata yake kukubaliana na matokeo waliyoyapata na kujipanga kufanya vizuri katika mashindano yajayo.

Timu ya Kata ya Mecco ndiyo iliyoanza kuziona nyavu za Timu ya Kata ya Shibula dakika ya 5 kupitia mchezaji wake Sylvester Godfrey, Kisha Timu ya kata ya Shibula kusawazisha goli hilo dakika ya 14 kupitia mchezaji wake Emanuel Lubala na baadae dakika ya 76 kuongeza goli la pili.

Mashindano haya yataendelea tena hapo kesho siku ya jumapili katika Uwanja wa Buswelu Sekondari kwa kuzikutanisha Timu ya Kata ya Nyakato na Timu ya Kata ya Bugogwa

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’

Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
08.09.2018












No comments:

Post a Comment