Watu
11 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya
barabarani iliyohusisha magari manne ikiwemo gari ndogo ya abiria aina
ya Toyota Hiace iliyotokea jana eneo la Mlima Igawilo Kasoko Jijini
hapa.
Kwa majibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa kumi na moja za jioni ambapo chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni kufeli kwa Lory lenye namba T334 DJN lililokuwa limebaba ndizi likitokea Wilayani Rungwe.
Amesema,
waliofariki dunia ni watu ni na idadi ya majeruhi bado haijapatikana
kwani watu waliokuwepo kwenye magari hayo walikimbizwa hospital kwa
ajili ya matibabu.
Aidha
amesema baada ya Lory namba T334 DJN likitokea Tukuyu, kufeli brek
hivyo kugonga gari Dogo ya abiria Hiace namba T883 ABS ambalo nalo
liligonga Lory lingine lililopakia ndizi nalo kugonga Lory la mafuta.
Amesema , majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajli ya matibabu.
Amesema , majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajli ya matibabu.
Baadhi
wa mashuhuda wa ajali hiyo, walisema kuwa dereva wa lory
lililosababisha ajali alifanya makosa kwani alipoona gari hilo limeferi
brek alikuwa na uwezo wa kulichepusha pembeni ili kuepusha ajali hiyo
ambayo ni kubwa.



No comments:
Post a Comment