Waziri
Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa hali ya uzalishaji wa mazao ya
chakula na upatikanaji wake nchini umeendelea kuimarika.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akitoa hoja ya
kuahirisha Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
kutangaza kuanza kwa mkutano ujao mnamo Novemba 6 mwaka huu.
Mhe.
Majaliwa amefafanua kuwa tathmini iliyofanyika mnamo mwezi Juni, 2018
imeonyesha kwamba uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa mwaka
2017/18 ni tani milioni 16.9 ambapo kati ya hizo tani milioni 9.5 ni
mazao ya nafaka na tani milioni 7.4 ni mazao yasiyo ya nafaka.
“Kutokana
na uzalishaji huo na kwa kuzingatia mahitaji ya chakula nchini ambayo
ni tani milioni 13.6, kutakuwa na ziada ya tani milioni 3.3 hivyo nchi
itajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 124,”alisema Waziri Mkuu
Majaliwa.
Mhe.
Majaliwa ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuwasihi wananchi kutumia
akiba hiyo ya chakula kwa uangalifu kwani zipo nchi jirani ambazo zina
uhaba mkubwa.
Vile
vile ameziagiza taasisi zote zinazosimamia elimu ya lishe na afya
kuongeza nguvu zaidi katika kutafuta mbinu bora na kutoa elimu kwa
wananchi ili kupunguza kiwango udumavu na utapiamlo hususan kwa watoto
wadogo.
Akizungumza
kuhusu upatikanaji wa pembejeo za kilimo nchini, Waziri Mkuu amesema
kuwa Serikali inaendelea kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa pembejeo
muhimu za kilimo kwa wakati ambapo katika msimu wa kilimo wa mwaka
2018/19 upatikanaji wa mbolea aina zote umefikia kiasi cha tani 215,207
wakati matarajio ya matumizi ya mbolea hiyo ni tani 485,000.
Aidha,
Serikali itahakikisha upatikanaji na matumizi sahihi ya viuatilifu kwa
mazao mbalimbali na kwamba kwa msimu wa mwaka 2018/19 Serikali imetenga
jumla ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kupambana na wanyama pamoja
na wadudu waharibifu.

No comments:
Post a Comment