Thursday, October 11, 2018

MJUMBE BARAZA KUU UVCCM TAIFA -MWANZA, ASEMA KIPINDI CHA KUENZI KUMBUKIZI ZA BABA WA TAIFA LAZIMA ZIENDE SAMBAMBA NA UAJIBIKAJI WA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI

Kuelekea tarehe 14/10/2018 Nuchukue fursa hii kuupongeza uongozi wa Serikali ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongera kwa kushirikiana na viongozi wote wa Wilaya zote kwa kazi kubwa za kupambana na maadui watatu ujinga,maradhi na  umasikini ambao hayati Baba wa taifa alipambana nao.Yapo makubwa mkuu wa Mkoa ameyafanya hususani katika kuleta maendeleo katika Mkoa wa Mwanza.

Nawapongeza wabunge wote wa Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na madiwani wao hakika kazi wanazifanya kila kona wanafanya  ziara kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Nawapongeza pia wakuu wa Wilaya kwa kusimamia kimikakati na kuimalisha suala la ulinzi na usalama katika Wilaya zetu.

Mwalimu alisema kazi ya kiongozi ni kuwaunganisha watu na kuwa kitu kimoja Mwanza yetu tu wamoja baina ya viongozi wa chama na serikali na wananchi wote

Vijana tutumie siku ya kumbukizi ya mwalimu  kufikilia ni kwa namna gani tutaendeleza umoja wetu katika Mkoa wetu na taifa kwa ujumla.

Vijana wengi tujikite katika kufanya kazi na tuepukane na dira ya kuwa chanzo cha kuvunja au kuharibu umoja wetu.

Tupinge
 Utabaka,Ukanda,Ukabila,
Udini.

Tuhimize umoja na mshikamo wa muungano wetu
Tanzania ni wamoja tutaishi kwa umoja na tutashiriki matukio kwa umoja wetu.

Umoja ndio ushindi na ulinzi wa amani ya Taifa letu

Mwisho
Dk John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndiye dira ya taifa letu na mzalendo wa kwanza kwa kupambana na maadui wa taifa hili na kulinda raslimali za taifa.
Vijana tuwe walinzi namba moja kwa Rais wetu kama alivyojitoa kuwa mzalendo namba moja katika Taifa.
SISI NI TANZANIA MPYA
Hapa kazi tu
Tukutane kazini

Kashilimu Juma Richard
Mjumbe baraza kuu uvccm Taifa.

No comments:

Post a Comment