Saturday, October 27, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mogella Ashiriki Fursa Mpya 2018 na Kuwaasa Vijana Kuchangamkia Fursa Mbalimbali Zilizopo Mkoani Mwanza

Semina ya Fursa Mpya 2018 inayoandaliwa na Clouds Media Group kila Mwaka , Leo hii wakazi wa Mwanza na watanzania kwa Ujumla  wamenufaika na Semina hii ambayo viongozi wa Kiserikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mogella na wasio wa kiserikali pia walikuwepo pamoja na uongozi wa Clouds Media Groups.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh John Mongella alipata nafasi ya kufungua semina hiyo aidha aliushukuru sana uongozi wa Clouds Media Groups kwakuleta Fursa Mkoani Mwanza kwani kila Mwaka huwa anajifunza vitu vipya. "Hakuna Maendeleo ya Jumla niya Mtu Mmoja mmoja, ni kama kifo" Alisema

Baada ya Ufunguzi, Semina iliendelea kama kawaida kwa kutoa mada tofauti tofauti na moja ya wachangiaji wa kwanza alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.John Mongella, Dkt Derick  C.E.O wa Uhuru Hospital na Patrick Tungu Mkurugenzi wa Taweso. Aidha Mkuu wa Mkoa alianza kwa kuitambulisha Geographia ya Mkoa wa Mwanza jinsi ulivyo na namna ulivyo kaa kifursa. Pamoja na mambo mengine Mkuu wa Mkoa ameeleza fursa zilizopo katika kutunza mazingira na Afya huku akiambatanisha na Kauli Mbinu Isemayo Usichukulie Poa Nyumba ni Choo

Baada ya hapo Mkurugenzi wa Uhuru Hospital pamoja na Mkurugenzi wa Taweso waliweza kuongea Mafanikio waliyoyapata na kuchangia Fursa zilizopo katika Afya pamoja na Technolojia .Aidha waliweza kuwaasa vijana kwamba Fursa zipo katika makundi makuu matatu.Moja ni katika Technolojia, pili ni katika Afya na Mwisho ni katika Agrobusiness.

Baada ya hapo Mada zingine ziliendelea ikiwemo swala la kilimo, wadau mbalimbali waliweza kushikiri katika kutoa au kufafanua Fursa zilizomo katika kilimo,Aidha moja ya mashahidi wameweza kuwaasa watu wasiogope kuanzisha kitu hasa wakipendacho.

Imetolewa na 

Katibu Hamasa na Chupukizi 
UVCCM Mkoa wa Mwanza
Hussein Kim















No comments:

Post a Comment