Saturday, October 27, 2018

MCHEZAJI CHIPUKIZI ALIYENG'ARA MICHUANO YA ANGELINE JIMBO CUP 2018 AENDA DENMARK KWA MAJARIBIO.

Mshambuliaji chipukizi aliyeng'ara katika mashindano ya Angeline Jimbo Cup 2018 akichezea Timu ya Kata ya Ibungilo Kelvin John ameenda nchini Denmark kwaajili ya majaribio ya kujiunga na klabu ya HB Koge inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini humo.

Kelvin amepata nafasi hiyo baada ya kufanya vizuri kwenye michuano maalumu ya kuwania kushiriki fainali za vijana chini ya umri wa miaka 17 Afrika (AFCON U17) kwa ukanda wa afrika mashariki maarufu kama CECAFA AFCO Qualifier Tanzania ikimaliza nafasi ya tatu na baadae kushiriki mashindano ya Angeline Jimbo Cup 2018 yaliyokuwa na lengo la kukuza na kuibua vipaji kauli mbiu ikiwa ni kuifanya michezo kuwa ajira yaliyofanyika ndani ya jimbo la Ilemela na kuasisiwa na mbunge wa jimbo hilo Mhe Dkt Angeline Mabula, Kelvin John akiibuka mchezaji bora katika mashindano hayo akiichezea timu ya kata ya Ibungilo.

Akiwa nchini Denmark Kelvin atapata wasaa wa kuitumikia Timu yake hiyo kwa majaribio yatakayochukua siku 18 kwa wastani wa wiki tatu huku akifuatiliwa na makocha wa timu hiyo.

Aidha mchezaji Kelvin John ameshukuru kwa kupata nafasi hiyo sanjari na kuwaomba waTanzania kuendelea kumuombea  huku akiahidi kupeperusha vyema bendera ya nchi.

Nae muasisi wa mashindano ya Angeline Jimbo Cup ambae pia ni mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kukishukuru kituo cha TANZANIA FOOTBALL HOUSE kinachowalea na kuwatafutia nafasi za kucheza mpira wa kulipwa nje ya nchi amempongeza mchezaji huyo kwa nafasi aliyoipata huku akimuasa  kujituma na kuwa na nidhamu ili aweze kutimiza ndoto zake sambamba na kuahidi kuendelea kuimarisha sekta ya michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuzidi kuibua vipaji vipya na kuendeleza vile vya zamani kwa kuifanya sekta hiyo ya michezo kuwa ajira rasmi

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga'


Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
27.10.2018.




No comments:

Post a Comment