Serikali
imesema italichukua na kulihifadhi kama kumbukumbu ya vitu alivyokuwa
anatumia hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, gari alilokuwa
akitembelea mwaka 1968 na kuundwa upya na Chuo cha Ufundi Stadi (Veta),
mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Dk. Ally Mohamed Shein, amesema hayo jana katika sherehe za kilele cha
mbio za Mwenge wa Uhuru baada ya kutembelea banda la Veta na kujionea
gari alilokuwa akitumia mwalimu wakati wa harakati zake za kutafuta
uhuru ambapo pia aliwapongeza vijana hao kwa umahiri wa kutengeneza gari
hilo.
“Vijana hao wameonyesha kwamba wamefuzu vizuri na wameonyesha uzalendo, Serikali inatambua mchango huo.
“Serikali
itaongeza vyuo vya ufundi Tanzania Bara na Visiwani kwa lengo la
kuhakikisha vijana wanapata fursa ya kujiunga na vyuo hivyo ili waweze
kujiajiri,” alisema Dk. Shein.

No comments:
Post a Comment