Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumbà na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula amepiga
marufuku ugawaji viwanja ambayo tayari vimemilikishwa huku wamiliki wake
wa awali wakitafutiwa eneo lingine.
Hatua
hiyo inafutia kushamiri kwa tabia iliyozueleka kwa baadhi ya watendaji
wa sekta ya ardhi katika halmashauri kugawa maeneo ambayo tayari yana
wamiliki wake kwa watu wengine wenye uwezo na baadaye kuwaahidi wamiliki
halali kuwapatia kiwanja kingine.
Mhe
Mabula alitoa kauli hiyo wilayani Musoma mkoa wa Mara mwishoni mwa wiki
alipokutana na watendaji wa sekta ya ardhi katika Manispaa ya Musoma
pamoja na halmashauri za wilaya za Musoma na Butiama wakati wa ziara
yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake aliyoyatoa wakati wa
ziara yake ya februari mwaka 2018.
"Kuanzia
sasa ni marufuku kwa watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri
kugawa viwanja 'pandikizi' katika maeneo ambayo tayari yameshamilikishwa
kwa mananchi kwani suala hili limekuwa likileta migogoro mikubwa katika
sekta ya ardhi" alisema Mabila.
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, suala
hilo limekuwa likijitokeza sana hasa maeneo yanayovutia na mara nyingi
linachangiwa na maafisa ardhi wasiokuwa waaminifu ambao humpatia mtu
mwenye uwezo kiwanja kilichomilikishwa kwa ahadi ya kumpatia mmiliki
halali kiwanja kingine.
Alisema,
serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ambayo
imekuwa ikiwatetea watu wa hali ya chini haitavumilia hali hiyo
iendelee kushamiri na kusema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa watendaji
wote wa sekta ya ardhi watakaoendelea au kubainika kufanya mchezo huo.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Angeline Mabula ameshangazwa na kasi ndogo ya utoaji hati za ardhi kwa
halmshauri ya wilaya ya Rorya ambapo jumlà ya hati 95 hazijapelekwa kwa
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Simiyu kwa ajili ya kukamilishwa
tangu Oktoba mwaka 2017.
Kamishna
Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Simiyu Godwin Tumaini alieleza kuwa
halmshauri hiyo imekuwa ukisusua katika kuwasilisha hati za ardhi katika
ofisi yake kwa ajili ya kuakamilishwa ili kugawiwa kwa wananchi na
kubainisha kuwa katika kipindi cha miezi mitatu ni hati moja tu ndiyo
iliwasilishwa katoka ofisi yake halmashauri ya wilaya ya Rorya.
Kufuatia
hali hiyo, Mabula amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Rorya
Charles Chacha kuwapangia maafisa ardhi watano wa halmshauri hiyo kila
mmoja kushughulikia hati tano kwa wiki jambo litakalofanya halmshauri
kutengeneza hati 35 kwa wiki.
Aidha,
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka watendaji
wa sekta ya ardhi kuwapa elimu wananchi wa Rorya kwa lengo la kupunguza
migogoro ya ardhi ambayo mingi imechangiwa na uelewa mdogo kwa
wananchi pamoja na migogoro ya kikabila na koo.
"Cha
msingi hapa ni kutoa elimu na siku nyingine mkienda kwa wananchi siyo
kwa ajili ya kutatua tu migogoro bali iwe pia kutoa elimu na kuepuka
masula ya siasa, haiwezekani katika wilaya ya Rorya kila eneo
linapotokea mgogoro wa ardhi basi lipelekwe jeshi hivyo elimu muhimu
sana kwa wananchi" alisema Mabula.
Mmoja
wa wakazi wa wilaya ya Rorya ambaye ni msaidizi wa mbunge wa Rorya Mzee
Majwala ameiomba serikali kusaidia kutoa elimu kwa wananchi wa wilaya
hiyo na kubainisha tatizo kubwa linaloikabili wilaya ya Rorya ni
migogoro inayohusisha makabila na koo na kutolea mfano wa makabila ya
Wasimbiti na Wajaluo ambapo alisema hata ukiitishwa mkutano wa
usuluhishi katika makabila hayo wanakuja watu wachache.
Mabula
amemaliza ziara yake katika mkoa wa Mara baada ya kutembelea wilaya za
Bunda, Serengeti, Rorya, Butiama na Musoma ambapo alifanikiwa kutatua
migogoro ya mipaka baina ya vijiji na vijiji, kushughulikia kero za
ardhi za muda katika maeneo hayo pamoja na kufuatia utekelezaji wa
maagizo yake aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya februari 2018.

No comments:
Post a Comment