Maadhimisho ya Sherehe za Kumkumbuka Baba wa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kufikia miaka 19 tangu kufariki kwake yaliyofanywa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ilemela kwa kufanya usafi katika kituo cha afya Buzuruga, kuona wagonjwa katika kituo hicho cha afya, kugawa msaada wa vyakula kwa wagonjwa, kusaidia shughuli za ujenzi unaoendelea katika kituo hicho na baadae kuzindua shina la umoja wa vijana katika mtaa wa Nyambiti yamemrudisha Katibu Mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kata ya Buzuruga na kuhamia Chama Cha Mapinduzi kufuatia kuvutiwa kwake na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Magufuli katika kusimamia haki, usawa, uadilifu, uwajibikaji na usimamizi mzuri wa rasilimali za nchi katika kuleta maendeleo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Comred Jamal Babu mara baada ya kumpokea kada huyo wa CHADEMA amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake vitaendelea kuyaenzi mawazo ya Mwl. Nyerere kwa kauli na vitendo huku akiipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli kwa utekelezaji mzuri wa Ilani inayovutia wapinzani kujiunga na chama chake ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, uimarishaji wa shirika la ndege, na uboreshaji wa huduma za afya
‘… Mawazo ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yapo hai na yatakuwa hai, Na sisi tutaendelea kuyaenzi katika kipindi chote kama ambavyo tunafanya sasa …’ Alisema
Aidha amewaasa viongozi wa CCM kwa ngazi zote kuhakikisha wanawajibika katika nafasi zao kwa kusimamia utekelezaji wa Ilani na uimarishwaji wa Chama kuanzia kwenye mashina na kwenye matawi.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Vijana UVCCM wilaya ya Ilemela Comred Nehemia Philemon amesema kuwa lengo la kuadhimisha kumbukizi hiyo ya tangu kufariki kwa muasisi wa taifa la Tanzania Mwalimu J. K Nyerere ni kuwakutanisha vijana pamoja na kuisaidia jamii katika shughuli za kimaendeleo kama ishara ya kuunga mkono yale yote mazuri yaliyokuwa yakifanywa na muasisi huyo huku akimshukuru mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula kwa ushirikiano alioutoa katika kufanikisha maadhimisho hayo.
Nae katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM wilaya ya Ilemela Comred Denis Kankono amesifu shughuli za maendeleo zinazotekelezwa ndani ya jimbo la Ilemela chini ya mbunge wa jimbo hilo Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kushirikiana na Serikali kuu ikiwemo ujenzi wa majengo ya maabara, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la upasuaji, jengo la mapokezi na nyumba ya mtumishi ujenzi unaoendelea katika kituo cha afya Buzuruga.
Katibu Mwenezi wa CHADEMA kata ya Buzuruga amejiunga na CCM katika sherehe hizo na kupokelewa na Mjumbe huyo wa halmashauri kuu ya CCM Taifa kwa madai kuwa amechoka siasa za kibaguzi na zisizokuwa na lengo la kumsaidia mtanzania huku akisifu na kuridhishwa na hatua anazochukua Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli katika kuwatumia wananchi wake na kuwaletea maendeleo.









No comments:
Post a Comment