14/10/2018 Mjumbe Baraza Kuu Uvccm Taifa aungana na mamia ya vijana katika kufanya usafi maeneo mbalimbali mjini Sengerema
Sambamba na kufanya usafi Ndg Kashilimu Juma Richard ameshiriki katika zoezi la kuchangia damu kwani ni ishara ya uzalendo mkubwa na ni miongoni mwa vijana wachache wenye kufanya zoezi hili.
Kupitia zoezi hili ni ibada tosha kwani hata Mungu anapenda na kuwainua wenye uwezo wa kujitoa kwa ajili ya kuokoa maisha ya ndugu zetu.
Wapo wahitaji wengi wa damu kama watoto wa chini ya umri wa miaka 5, wanaopata ajali, lakini Wapo wanaotakiwa kuongezwa damu kutokana na matatizo mbalimbali
Kupitia zoezi hili tutaweza kupunguza vifo vya watoto na mama zetu wanaopoteza maisha na damu vipindi vya kujifungua.
Mjumbe baraza kuu awataka vijana waendelee kujitoa hasa katika zoezi la kizalendo lenye tija kwa taifa na wananchi kwa ujumla.
Mwisho
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere atakumbukwa na ataendelea kukumbukwa kwa taifa,Africa na Dunia yote.
Mungu ampumzishe kwa amani
Tanzania tunaumia kumpoteza shujaa ila kazi ya Mungu haina makosa
Kashilimu Juma Richard
Mjumbe baraza kuu uvccm Taifa







No comments:
Post a Comment