Chuo
cha Ufundi Stadi (VETA) kimemuenzi Baba wa taifa Mwalimu Julius
Nyerere, kwa kulifanyia ukarabati gari alilokuwa akilitumia wakati wa
harakati za kutafuta Uhuru wa Tanganyika.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA Nchini, Dk. Pancras Bujulu,
wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani
Tanga.
Dk.
Bujulu amesema wameamua kulikarabati gari hilo ili kumuenzi hayati
Mwalimu Nyerere, ambapo kazi hiyo imefanywa na vijana wanaopata mafunzo
ya ufundi stadi kutoka Moshi, mkoani Kilimanjaro.
“Gari
hilo aina ya Austene yenye namba ya usajili MS 5480, inahisiwa
lilitengenezwa mwaka 1947, lilikuwa limehifadhiwa kwenye ofisi ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kilimanjaro.
“Kwetu
ilikuwa kama fursa kwa vijana wetu kuonyesha namna walivyoiva kwenye
ufundi tukaliomba na kupatiwa na kwa sasa tumelitengeneza na
linatembea,” amesema mkurugenzi huyo.
Kwa mujibu wa Dk. Bujulu, gari hilo lilitumiwa na Mwalimu Nyerere mwaka 1961 wakati wa harakati za kutafuta uhuru.
Gari hilo linatarajiwa kukabidhiwa kwa Serikali Oktoba 14, siku ya kilele cha maonyesho hayo.

No comments:
Post a Comment