Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’
alitekwa jana alfajiri Oktoba 11, 2018 jijini Dar es Salaam kwenye
Hoteli ya Colosseum iliyopo Oysterbay alipokwenda kwa lengo la kufanya
mazoezi.
Akizungumzia
tukio hilo jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro
Mambosasa amesema katika uchunguzi wao wa awali kupitia kamera za
ulinzi (CCTV) zimeonyesha magari mawili yalihusika.
Mambosasa amesema katika tukio hilo magari hayo mawili yalifika hotelini hapo kabla MO hajafika.
Amesema
gari ya kwanza aina ya Toyota Surf ilikuwa imeegeshwa nje ya geti la
kuingilia hotelini likiangalia usawa wa ndani ya hoteli, huku la pili
aina ya Toyota Noah likiegeshwa pembeni kidogo ya eneo ambalo MO hupaki
gari lake kila afikapo hotelini na kushuka.
Wakati Mo akifika hapo kamera zilionyesha gari ya ndani aina ya Noah ikiiwashia taa gari ya nje kuashiria kwamba Mo amefika.
Mara
baada ya kuwasha taa hizo wakati Mo anashuka watu wawili raia wa kigeni
(Wazungu) waliteremka na kuingia ndani ya geti la kuingilia kisha
kukutana na Mo akiwa anafunga gari yake na kuanza kuingia ndani ya
jengo.
Watu
hao wawili walifika kwa Mo na kufanikiwa kumbana vizuri ambapo wakati
wakiendelea na kazi hiyo gari iliyopaki nje ilikuwa imeshafanikiwa
kuingia ndani ya geti na watekaji kufanikiwa kumuingiza katika gari
iliyotoka nje aina ya Surf.
Mara
baada ya watekaji kufanikiwa walimpokonya funguo ya gari na simu yake
kisha kuzitupa chini na kuanza safari ya kuondoka eneo hilo.
Kamera
zilionyesha tukio hilo lilikamilika majira ya saa 11:35 alfajiri ambapo
wakati wanatoka, Surf ambayo ilimbeba Mo ilitangulia mbele huku Noah
ikifuata nyuma mpaka kwenye geti la kutokea.
Walipofika
hotelini hapo Wazungu hao, alishuka mmoja na kufyatua risasi mbili juu
kuamrisha mlinzi afungue geti ambapo wakati walinzi wakijisalimisha
Mzungu aliyeshuka akakimbia getini na kufungua geti mwenyewe na gari
zote kufanikiwa kukimbia.

No comments:
Post a Comment