Ni
masaa 24 toka bilionea kijana Mo Dewji atekwe na watu wasiojulikana
jana Alhamisi akiwa GMY ya hotel ya Colosseum Oysterbay jijini Dar es
salaam na mpaka muda huu hakuna taarifa mpya.
Taarifa ya mwisho jana kutoka kwa Kamanda
wa Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ilisema watu
wanaoshikiliwa kwaajili ya mahojiano kutokana na tukiohilo ni 12.
Mambosasa alisema kuwa watu hao wanashikiliwa ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo , kati ya hao waliokamatwa ni pamoja na walinzi wa hoteli ya Collesium, mahali ambapo tukio hilo lilitokea.
Mambosasa alisema kuwa watu hao wanashikiliwa ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo , kati ya hao waliokamatwa ni pamoja na walinzi wa hoteli ya Collesium, mahali ambapo tukio hilo lilitokea.
Akizungumza
jana na Clouds Fm, dereva wa Mo Dewji alisema kuwa lilikuwa ni jambo
la kawaida kwa mfanyabiashara huyo tajiri kuendesha gari lake mwenyewe
kwani alikuwa anaamini ana amani.
“Mo
Dewji ni tajiri lakini anaishi maisha fulani hivi kama vile sio tajiri.
Yaani alikuwa hana hofu na raia kwa sababu yeye kila mtu anayekutana
naye ni kama vile anajuana naye miaka mingi,” alisema.
Dereva
huyo ambaye amefanya kazi kwa Mo tangu mwaka 2001 ameeleza kuwa Mo
alikuwa anajiamini na hakuwa na uoga dhidi ya raia, lakini aliwahi
kumtahadharisha mwaka huu kuwa amekuwa akipokea jumbe za vitisho.

No comments:
Post a Comment