Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewataka vijana kuacha tabia ya kuchagua kazi na
badala yake wachangamkie fursa zinazojitokeza katika utekelezaji wa
miradi mikubwa inayoendeshwa na Serikali ikiwemo ya ujenzi.
Miradi
hiyo ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme, ujenzi wa
barabara, upanuzi wa bandari na ujenzi wa miundombinu ya nishati.
Majaliwa
ametoa rai hiyo leo Jumatano Oktoba 24, 2018 wakati wa maadhimisho ya
miaka 73 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) ambayo kwa mwaka huu
yamebebwa na ujumbe ‘Uwezeshaji wa vijana na ubunifu katika kufikia
malengo ya maendeleo endelevu’.
Majaliwa
amesema Serikali inatambua uwepo wa changamoto ya ajira sababu
iliyoifanya kuanzisha mikakati mbalimbali ambayo inawajengea uwezo
vijana.
Miongoni mwa mikakati hiyo ni kuanzisha wakala wa ajira, mafunzo ya kazi kwa vijana na sera ya ajira.
Amesema
pamoja na mikakati hiyo bado kuna changamoto ya ajira hivyo ameiomba UN
kuwapa nafasi za ajira, mafunzo kwa vitendo na fursa za kujitolea
zinapojitokeza.
Awali,
alipowasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
yalipofanyikia maadhimisho hayo, Waziri Mkuu alikagua gwaride
lililoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).


No comments:
Post a Comment