Watu
sita akiwemo mtoto mchanga wa jinsia ya kike wamefariki dunia na
wengine saba kujeruhiwa katika ajali iliyotokea kijiji cha Msata,
barabara kuu ya Segera/Chalinze mkoani Pwani.
Akithibitisha,
kamanda wa polisi mkoani Pwani Naibu Kamishna wa Polisi ACP Wankyo
Nyigesa alisema kwamba ajali hiyo imetokea Novemba 5, 2018 majira ya saa
moja usiku baada ya gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster
ikitokea Mkata kwenda Mbezi -Dar es salaam kuligonga kwa nyuma lori
namba KBV 746C/ZE2861 FAW iliyokuwa imeegeshwa barabarani kutokana na
kuharibika.
Amesema dereva wa Toyota coaster iliyosababisha ajali ambae hajafahamika jina lake alikimbia baada ya kutokea ajali.
ACP
Wankyo alieleza kuwa waliopoteza maisha ni wanaume watano wenye umri
kati ya miaka 30-40 ambao majina yao bado kufahamika. Alisema ,watu saba
walipata majeraha kwenye maeneo mbalimbali ya mwili yao .
"Waliopata
majeraha ni pamoja na wanaume wanne na wanawake watatu ambao wote
wamepelekwa zahanati ya jeshi Kihangaiko -RTS na kituo cha afya Lugoba
kwa matibabu zaidi "alisema Wankyo, akiongeza kuwa miili ya marehemu
imehifadhiwa hospital ya wilaya ya Bagamoyo kwa uchunguzi wa daktari.
Alitaja
chanzo cha ajali, ni uzembe wa dereva wa gari namba T. 124 DHW aina ya
Toyota coaster kujaribu kulipita bila tahadhari gari jingine lililokuwa
limeegeshwa baada ya kuharibika na wanaendelea kumsaka.
Kamanda
huyo alitoa rai kwa madereva kutii sheria za usalama barabarani na
kuacha tabia za kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi ili kuepukana
na ajali zembe.
Wankyo
aliwapa salamu madereva hao, kuwa hawatakuwa na muhali nao kwani
watakamatwa na kuwachukulia hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa
wengine.

No comments:
Post a Comment