Tuesday, November 6, 2018

MHE. MABULA AWEZESHA TAULO ZA KIKE KWA WASICHANA 1000 SHULE YA SEKONDARI BUHONGWA NYAMAGANA

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ametoa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike 1000 shule ya bweni Buhongwa sekondari iliyopo kata ya Buhongwa Wilayani Nyamagana. Ikiwa ni mkakati maalum wa Mhe. Mabula kumwezesha mtoto wa Kike kuhudhuria vipindi vyote vya darasani muda Wote hata siku za hedhi, kwa ushirikiano na taasis tanzu ya First Community Organizations pamoja na Business Professional Women kwa udhamini wa wawekezaji wazawa Lulu Pads.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mbunge Jimbo la Nyamagana, Rais wa taasis ya Business and Profession Women tawi la Tanzania Bi. Betila Masawe Mongella ambaye pia ni mke wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, amesema mtoto wakike anayetoka familia duni ana hatari ya kukosa masomo kwa  kwanzia siku 36 hadi 72 kwa mwaka ili kujistili nyumbani katika siku za mzunguko wake wa hedhi. Kadharika Mama Betila amemtangaza Magreth Fidelis mwanafunzi shule hiyo kidato cha tatu mchepuo wa Sayansi kuwa ndio balozi wa BPW pamoja na First Community Organisation katika Kampeni za uwezeshaji wa towel za kike kwa wanafunzi kike wilayani Nyamagana pamoja na mataifa 198 wanachama wa BPW.

Naye mwenyekiti wa taasis ya First Community Ndg. Ahmed Misanga ameshukuru ushirikiano tanzo wa taasis yake na taasis BPW ambao umekuwa chachu katika zoezi la ugawaji wa taulo za kike kwa shule nane za mkoa wa Mwanza na shule mbili Wilayani Nyamagana kwa ushirikiano na Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula pamoja na wawekezaji wazawa Lulu Pads ambao wamekubali kuwekeza katika sekta ya elimu katika ugawaji wa taulo za Kike. Wakati huo huo Ndg. Kheri katibu wa Mbunge Jimbo la Nyamagana ametumia adhara hii kuwahakikishia wanafunzi wa kike kuwa zoezi hili ni endelevu na linatazamiwa kuzifikia shule zote za Sekondari wilaya ya Nyamagana.

Hafla hii  imehudhuliwa na Katibu wa Mbunge Jimbo la Nyamagana, ujumbe wa taasis  mbili tanzu First Community Organizations pamoja na Business and Profession Women, Diwani kata ya Buhongwa, uongozi wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Buhongwa, mtendaji wa serikali Kata pamoja na uongozi wa shule, sanjari na utoaji wa elimu ya Afya ya uzazi kutoka kwa Madktari Bingwa Dkt Florah Chacha, Dkt Amina, mhamasishaji jamii Bi Didas Vitenge pamoja na Mnasii Bi Florah B. Magabe.

Imetolewa na 
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana






No comments:

Post a Comment