Tuesday, May 28, 2019

MHE DKT ANGELINE MABULA AIWAKILISHA NCHI MKUTANO UN-HABITAT

Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula ameiwakilisha nchi ya Tanzania katika mkutano wa 27 wa nchi zaidi ya 150 wanachama za Umoja wa Mataifa kupitia Baraza la Umoja huo linalosimamia mazingira duniani (UN-HABITAT) ulioanza Mei 27, 2019 na kuisha Mei 31, 2019.

Mkutano huo unaofanyika katika makao makuu ya baraza la mazingira la umoja wa mataifa yaliyopo Gigili, Nairobi nchini Kenya utajadili masuala mbalimbali yanayohusu Makazi, Uendelezaji Miji na Ustawi wa Jamii kwa ujumla wake ambapo nchi ya Tanzania ilipokea mwaliko wa kufanya mawasilisho ya mradi wa mfano unaoendana na kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu inayosema ‘ Innovation for better quality of lives in cities and community’  ambapo mapendekezo hayo tayari yamepokelewa  na mradi wa ‘Ubunifu katika kupima na kumilikisha ardhi katika makazi yasiyorasmi Tanzania’ kwa kutumia simu ya mkononi (Mobile App) umebuniwa huku ukitarajiwa kuanza kutumika kwa mkoa wa Dar es Salaam kabla ya kuendelea nchini kote.


' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '


Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
27.05.2019.






No comments:

Post a Comment