Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa ,na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Seleman Jafo, amesema hadi sasa shule za sekondari 1,241
zimejengewa mabweni kati ya shule za sekondari 3,634 zilizopo kwa
kutumia ruzuku kuu.
Jafo
amesema hayo leo Jumatatu Mei 27, bungeni jijni Dodoma, wakati akijibu
swali la Mbunge wa Viti Maalum, Azza Hilaly Hamad (CCM).
Katika
swali lake, Azza alihoji serikali ina mkakati gani wa kujenga mabweni
katika shule za sekondari zilizoanzishwa kitarafa ili kuwasaidia watoto
wa kike kupata elimu bora.

No comments:
Post a Comment