Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amewahakikishia wananchi kuwa Jimbo la Ilemela litaendelea kuwa tanuru la kuoka vipaji vya Michezo mbalimbali na kuwa tegemeo kwa nchi.
Kauli hiyo ameitoa wakati akifunga mashindano ya Ramadhan Cup 2019 yaliyoanza Mei 05, mwaka huu katika kiwanja cha Magomeni kata ya Kirumba na kuhusisha timu zaidi ya 12 kutoka kata tofauti za jimbo hilo kwa lengo la kuendeleza vipaji na kutoa fursa kwa vipaji vipya ambapo amewataka wadau wa Michezo kushirikiana kwa pamoja kuanzisha mashindano ya kimichezo itakayosaidia kuzalisha wachezaji tegemezi kwa taifa huku akielezea historia za wachezaji mbalimbali waliotokea jimbo la Ilemela akiwemo Kelvin John, Mrisho Ngasa, Henry Joseph, Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Obadia Mugusa na Mwinyi Kazimoto waliotokana na mashindano kadha wa kadha yanayofayika jimboni humo ikiwemo yale ya Ilemela Jimbo Cup.
‘.. Niwaombe wadau wengine kuendelea na moyo kama huu wa kuanzisha mashindano tofauti kama mwaka huu tulivyo na Ramadhana Cup, kipindi chengine tuwe na ya Pasaka, Christmass au mashindano yoyote yale hata ya kijamii ili mradi tupate vipaji vipya na tegemezi kwa nchi, Na mie nitakuwa pamoja nanyi ..’ Alisema
Akimkaribisha mbunge huyo, mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Dkt Severine Lalika ametoa kiasi cha fedha shilingi laki mbili kama ishara ya kuunga mkono jitihada za kuibua vipaji vya michezo na kuviendeleza vile vya zamani huku akiwahakikishia ushirikiano wadau wote walioteyari kuanzisha mashindano ya kimichezo ndani ya wilaya hiyo.
Kwa upande wake mratibu wa mashindano hayo Comred Denis Kankono mbali na kumshukuru mbunge wa Jimbo hilo kwa kuunga mkono mashindano ya Ramadhan Cup 2019, amempongeza kwa namna anavyojitoa katika kuimarisha Michezo ndani ya jimbo lake ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama chake CCM.
Fainali ya mashindano ya Ramadhan Cup 2019 ilihusisha Timu ya Kirumba Boys dhidi ya Beach Boys ambapo Timu ya Kirumba ilifanikiwa kuichapa Timu ya Beach Boys goli moja kwa sifuri, Goli lililofungwa na Mchezaji Isaac Micah Kachwere dakika ya pili na kuifanya Timu hiyo kupata zawadi ya Kombe, Mbuzi mmoja, Jezi seti moja na mpira huku mshindi wa pili akipata Mbuzi mmoja, Jezi seti moja na mpira.
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
June 07, 2019.







No comments:
Post a Comment