Friday, June 7, 2019

KATIBU MKUU CCM TAIFA AFUNGA MASHINDANO YA STANSLAUS MABULA RAMADAN CHAMPIONSHIP CUP 2019

 Na Chief Missanga

Mhe. Dkt. Bashiru Ally Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi afunga rasmi mashindano ya Stanslaus Mabula Ramadan Championship Cup mwaka 2019, ambapo kikosi cha La Family kutoka Ilemela kuimebuka kidedea kwa mikwaju ya penati tatu kwa mbili dhidi ya upinzani wake Uhuru Rangers kutoka Nyamagana. 

Mhe. Dkt. Bashiru akiwakilishwa na Mjumbe Kamati Kuu CCM taifa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe. Kheri James ametoa salamu za Mhe. Dkt. Bashiru kwa kupongeza hatua kubwa inayofanywa na Mbunge Jimbo la Nyamagana kwa kuwaleta wananchi pamoja kupitia michezo ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Kadharika Mhe. Kheri amehimiza vijana kuboresha afya zao kupitia michezo kwani inachochea  utalii, afya pamoja na kukuza, kuibua vipaji sanjari na kuwezesha ajira.

Naye Mbunge  Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ameshukuru vikosi vyote 14 kushiriki mtanange huo kutoka wilaya ya Nyamagana  na Ilemela kupitia uratibu wa JUVIKIBA Jumuiya ya Vijana Kislamu BAKWATA pamoja na UVCCM Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Mirongo na yeye kudhamini miaka mitatu mfululizo. Mhe. Mabula amemwambia mgeni rasmi kuwa ameendelea na ufadhiri wa michuano mbali mbali ikiwemo michuano ya Kata, Ligi daraja na nne, mchezo wa Draft, na amekuwa akifadhili vifaa vya michezo mashuleni, Vikosi vya kata pamoja vilabu mbali mbali.

Akitoa shukurani kwaniaba ya wananchi naibu Mayor wa halmashauri ya Jiji la Mwanza Ndg. Kotecha ametumia adhira hiyo kumpongeza Mhe. Mabula kuwa kiongozi wenye dhamira ya dhati kuinua michezo wilayani Nyamagana na kufadhiri michuano hiyo kwa miaka mitatu mfululizo. 

Zawadi zilizokabidhiwa  ni pamoja na Ng'ombe Mnyama, mipira Moya miwiki na Kombe kwa mshindi wa Kwanza  kikosi cha La family alichoibuka kidedea na mabingwa watetezi Uhuru Rangers ambao hawakufukuta na kuwa washindi wa pili walipata Mbuzi wawili Mpira mmoja, na mshindi watatu Mji mwema kupokea Mbuzi mmoja pamoja na Mpira. Zawadi zingine zilizokabidhiwa ni vyeti kwa vikosi vyote vishiriki,  Ngao kwa Mchezaji Bora, mfungaji Bora, Kikosi chenye nidhamu, na kipa Bora.  

Hafla hii ya uzinduzi imehudhuliwa na vikosi vyote 14 vishiriki, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ambaye Afisa Michezo Jiji Ndg. Bitegeko, Mwenyekiti wa taasis ya First Community Organisation na Mwenyekiti wa mashindano hayo Ndg. Ahmed Misanga, watendaji wa ofisi ya Mbunge Jimbo la Nyamagana, uongozi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya na Kata ya Mirongo wakiongozwa na Mwenyekiti UVCCM wilaya ya Nyamgana Mhe. Magori, uongozi wa JUVIKIBA Jumuiya ya Vijana Kislamu BAKWATA Mkoa na wilaya.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge 
Jimbo la Nyamagana





No comments:

Post a Comment