Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amefurahishwa na kupongeza uandaaji wa mashindano ya Marandu Cup 2019 yenye lengo la kuunga mkono jitihada za mbunge huyo katika kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya Michezo.
Hayo yamebainishwa wakati alipotembelea viwanja vya shule ya msingi Bugogwa kushuhudia mashindano hayo yaliyo katika hatua ya makundi ambapo amempongeza mdau Marandu Marandu kwakuanzisha mashindano hayo huku akiwataka wadau wengine kuona haja na kuiga mfano huo kwa kuanzisha mashindano mengine kwa michezo tofauti tofauti ili kuzalisha vipaji vipya.
Aidha Mhe Dkt Mabula amewahakikishia wananchi waliojitokeza kushuhudia mashindano hayo kuwa ataendelea na utaratibu wake wa kuendelea na mashindano ya Jimbo Cup kama mashindano makuu ya Jimbo katika kuibua vipaji, kukuza, kuviendeleza na kuifanya sekta ya Michezo kama sehemu ya kujiajiri na kujiendeleza kiuchumi.
Kwa upande wake mratibu wa mashindano hayo, Ndugu Almas amesema kuwa mashindano ya Marandu Ndondo Cup 2019 yalianza mapema mwezi huu na yanatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi June, 2019 yakikutanisha Timu 16 kutoka maeneo tofauti tofauti ya mkoa wa Mwanza ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya ng’ombe wa nne, mbuzi mmoja na jezi seti moja, mshindi wa pili atapata ng’ombe wa tatu, mbuzi mmoja na jezi seti moja huku mshindi wa tatu akipewa ng’ombe mmoja.
'Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga'
Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
June 11, 2019.





No comments:
Post a Comment