Wilaya ya Nyamagana imeweka mkakati madhubuti utakaowezesha changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa vipatavyo 9,800 pamoja na Matundu ya vyoo 12,000 inatatuliwa haraka ili kutekeleza elimu bila malipo kwa wanafunzi wa shule za awali hadi Sekondari Ifikapo 2020.
Hayo yamebainishwa na Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana akiwa ameambatana na mwenyeji wake Diwani Kata ya Luchelele, katika mkutano wa hadhara Kata ya Luchelele Mtaa wa Ngaza ikiwa ni mwendelezo wa kufikia mitaa 175 ya halmashauri ya Jiji la Mwanza. Mhe. Mabula amesema, serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inatumia takribani Sh. 23.7 Bill katika mpango wa elimu bila malipo ikiwa Nyamagana pekee inapokea takribani Sh. 1,200,000,000.00 kila mwaka. Mpango ambao umepelekea kuwa na ongezeko la wanafunzi na kusababisha uhaba wa Vyumba vya madarasa 9,800 pamoja na Matundu ya Vyoo takribani 12,000.
Mhe. Mabula amefafanua kuwa, tayari halmashauri ya Jiji la Mwanza imenunua kiwanda cha kufyatua Matofari chenye uwezo wa kufyatua matofari 4,000 hadi 8,000 kwa siku ili kukabiliana na changamoto hiyo. Ambapo wananchi wanapaswa kujenga msingi wa darasa na halmashauri ya Jiji kujenga ukuta na kisha serikali kuu kuezeka. Mhe. Mabula ametumia adhira hiyo kuwaambia wananchi wa Nyamagana, kuwa serikali imepokea msaada wa ujenzi wa vyoo vya Kisasa 20 kwa shule 20 na choo kimoja kitajengwa Kata ya Luchelele katika shule ya Msingi Luchelele.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana






No comments:
Post a Comment