Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amevitaka vyama vya wafanya biashara na wajasiriamali wanawake kutoka mikoa yote nchini kuiga mazuri yanayofanywa na chama cha wafanya biashara wanawake cha mkoa wa Mwanza (Tanzania Women Chamber of Commerce).
Rai hiyo ameitoa wakati akifunga maonesho ya kibiashara katika viwanja vya jengo la biashara mkoa wa Mwanza (Rock City Mall) yaliyoandaliwa na chama cha wafanya biashara wanawake mkoani humo yenye kauli mbiu ‘Mwanamke Jikomboe Kiuchumi’ yakikutanisha wafanyabiashara wanawake kutoka mikoa 6 kati ya mikoa ya nchi nzima iliyokuwa imelengwa, kwa muda wa siku Kumi ambapo amekipongeza chama hicho kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuhakikisha wanawajengea uwezo, wanawaunganisha, wanawatafutia mikopo na masoko ya bidhaa wanazozizalisha ili kujikwamua kiuchumi na kufikia malengo ya Serikali ya kuwa na uchumi wa kati kwa sera ya viwanda
‘.. Nimesikia maonesho haya ni ya kwanza kufanywa na TWCC mkoa wa Mwanza, Kwakweli mmethubutu na mnastahili pongezi, Niwaombe tu nyie mliotoka mikoa mingine muige mazuri haya ya Mwanza ..’ Alisema
Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka wafanya biashara hao kutumia katazo la Serikali la uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki kama fursa ya kujikwamua kiuchumi kwa kuzalisha mifuko mbadala yenye ubora na kwa gharama nafuu sambamba na kuwambusha juhudi za Serikali ya awamu tano chini Rais Mhe Dkt John Magufuli ikiwemo kuweka mazingira rafiki kwa taasisi za Serikali zinazosimamia ubora TBS na TFDA ,kuhuisha sheria zote zinazoonekana sio rafiki kwa maendeleo na kuondoa kodi kero.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi, Bi Jackline Budodi mbali na pongezi amesema kuwa chama hicho kilianza na wanachama 15 na mpaka sasa kina wanachama 106 huku akimuomba mgeni rasmi kuwasaidia kiwanja kwaajili ya ujenzi wa ofisi za chama hicho na jengo la biashara kama kitega uchumi.
Akihitimisha mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wanawake mkoa wa Mwanza, Bi Mariam Munaka ameishukuru manispaa ya Ilemela kwa kukubali kudhamini maonesho hayo na kumpongeza Dkt Mabula kwa kukubali kuja kuyafunga.
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga'
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela














No comments:
Post a Comment