Friday, June 14, 2019

MWENYEKITI WA CHIPKIZI MKOA WA MWANZA AFUNGA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU YA VIJANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 14

Mwenyekiti wa chipkizi wa umoja wa vijana mkoa wa mwanza ndugu Maria K Kahungwa  leo tarehe 14/6/2019
*Alialikwa kuwa mgeni rasmi katika fainali za mpira wa miguu ya watoto wenye umri chini ya miaka14(CHIPKIZI)

Mashindano hayo yameandaliwa na kuratibiwa na mkufunzi wa chipkizi wilaya ya ilemela na Comrade Mtoro

Jumla ya timu zipatazo tano (5) zilishiriki katika mashindano hayo yaliyo dumu kwa mda wa siku tatu

Timu zilizo shiriki fainali ni timu za MZALENDO NA HAPA KAZI

MZALENDO NDIO TIMU ILIYO IBUKA KIDEDEA NA KUCHUKUWA KOMBE

Akiongea na wachezaji mgeni rasmi wa fainali hizo binti Maria K kahungwa ambae ni mwenyekiti wa chipkizi mkoa wa mwanza amewaomba wazazi wajenge utamaduni wa kuwaruhusu watoto washiriki michezo mbalimbali mana michezo ni afya,ajira na  huleta mshikamano

katibu hamasa ,chipkizi, sera na utafiti UVCCM mkoa wa mwanza

HUSSEIN A KIMU
TUKUTANE KAZINI








No comments:

Post a Comment