Mapema leo tarehe 12/6/2019
Mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa mwanza Comrade Jonas Lufungulo
aliwaongoza wajumbe wa kamati ya UTEKELEZAJI ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wilani UKEREWE
Ziara hiyo imelenga kukutana na mabaraza yote ya kata katika maeneo yao au katika kata zao husika
ikiwa lengo ni
Kukaguwa uhai wa jumuiya,
kuwahamasisha vijana na wana ccm wote kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019
kuwajengea uwezo wa kiuchumi vijana kwa kuwaelekeza kujituma katika kufanya kazi na kuunda vikundi vya ujasilia mali ,kuwa wabunifu (creativity)
Kuunga mkono jitiada za mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Taifa Dr Josefu Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazo zifanya za kuwatumikia watanzania wote kwa moyo wa uzalendo
Nae mtendaji mkuu wa jumuiya mkoa wa mwanza Comrade Denis Luhende amehimiza kwa vijana wa ccm kuwa na utii wa bila shuruti pindi wanapopewa maelekezo na viongozi wao
katika ziara hiyo vijana wamejitokeza kwa wingi na kutowa kero zao na changamoto zinazo wakabili na kutolewa ufumbuzi jambo ambalo limewapa faraja kubwa sana na kutowa pongezi kwa ziara hiyo ya viongozi wa jumuiya ya vijana mkoa wa mwanza
KATIBU WA UHAMASISHAJI ,CHIPKIZI,SERA NA UTAFITI
UVCCM MKOA WA MWANZA
HUSSEIN A KIMU
TUKUTANE KAZINI

















No comments:
Post a Comment