Serikali
kupitia wizara afya ,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto imeandaa
mwongozo wa msamaha kwa makundi tofauti yasiyokuwa na uwezo ikiwa ni
pamoja kundi la watu wagonjwa sugu ikiwa ni pamoja na selimundu
Hayo
yamesemwa Juni 10 ,2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya jamii ,jinsia,wazee na Watoto,Dokta Faustine
Ndugulile,wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Taska Mbogo
aliyehoji mpango wa Serikali wa kuwasaidia wagonjwa wa Selimundu[Sickle
cell] juu ya kupata matibabu bure.
Katika
Majibu yake,Mhe,Ndugulile amesema wagonjwa wa Selimundu wanahitaji
matibabu mfululizo kwani huwa wanapata maumivu na madhara ya ugonjwa
huo mara kwa mara hivyo ,serikali imeandaa mwongozo wa kutoa msamaha
kwa makundi tofauti yasiyo na uwezo ikiwa ni pamoja na kundi la
wagonjwa wa Selimundu na kinachotakiwa ni kuhakikiwa na kupatiwa kibali
cha huduma bila malipo.
Aidha,Dokta.
Ndugulile amesema Serikali imeanzisha mpango wa Taifa wa Udhibiti wa
Magonjwa yasiyoambukizwa ambapo ugonjwa wa Selimundu [sickle Cell]
utakuwa ni moja ya magonjwa yatakayokuwa yanaratibiwa kitaifa.

No comments:
Post a Comment