Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema wakimbizi 66, 148
kutoka nchi mbalimbali wamerejeshwa katika nchi zao kati ya mwaka 2017
na Aprili 2019, wakiwemo 31,643 wa Burundi.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Masauni, Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu
swali la mbunge wa Viti maalum (CUF), Rukia Kassim Ahmed aliyetaka
kujua ni lini Serikali ya Tanzania itawarejesha nyumbani wakimbizi
waliojaa katika magereza mbalimbali nchini.
Masauni
amesema Mkoa wa Kigoma ndio una magereza zenye idadi kubwa ya
wakimbizi, “Wapo 91 na kati yao wafungwa ni 38 na mahabusu 53. Wakimbizi
ambao wamefungwa gerezani wanarejeshwa katika nchi zao za asili baada
ya kumaliza kutumikia vifungo vyao.”

No comments:
Post a Comment