Wabunge wanaoahidi na kutekeleza ahadi zao ni wachache Sana, Wengi wamekuwa wakiahidi na baada ya kupata dhamana ya kuongoza Umma wanasahau kutekeleza ahadi zao walizozitoa na wengine hata ile ilani ya uchaguzi iliyowapa nafasi hawaitekelezi.
Kauli hiyo imetolewa na Ndugu Ally Mambile , Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ukerewe wakati wa ziara ya Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mwanza katika wilaya hiyo, Mhe Lwota Kemilembe juu ya kuimarisha chama na jumuiya ya umoja wa wanawake UWT, Kutekeleza shughuli za maendeleo na kusikiliza kero na changamoto za wananchi kabla ya kuzipatia ufumbuzi ambapo amemshukuru Mbunge Kemilembe kwa msaada wake wa mifuko ya Saruji 50 na mabati 100 ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa kuhakikisha ofisi ya CCM wilayani humo inakarabatiwa upya baada ya kukaa kwa muda mrefu bila maboresho jambo linalochangia watendaji, viongozi na wananchama kufanya kazi ya ujenzi wa chama katika mazingira magumu na hatarishi kutokana na uchakavu wa jengo hilo la ofisi za wilaya
'.. Niseme tu kina mama wa Ukerewe hapa hamkukosea, Mlifanya uamuzi sahihi Sana maana wabunge wanaoahidi na Kutekeleza ahadi zao ni wachache Sana, Lakini kwa Mhe Kemi ni tofauti Sana yeye anaahidi na anatekeleza kile alichokiahidi ..' Alisema
Aidha Mwenyekiti Mambile amewataka wanachama wa CCM kupitia jumuiya hiyo kuhakikisha wanakuwa wamoja na kuandaa mikakati itakayoleta ushindi kwa chama chao.
Kwa upande wake Mbunge Lwota Kemilembe mbali na kushukuru kwa pongezi zilizotolewa juu yake, amewahakikishia wananchi na wanaCCM wa wilaya ya Ukerewe ushirikiano katika kupambana na changamoto zinazowakabili pamoja na kuwaasa wanawake wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, kugombea nafasi za Uongozi katika uchaguzi wa Serikali za mtaa na kuwaahidi kushirikiana nao katika chaguzi hizo zinazotaraji kuanza hivi karibuni.
Akihitimisha Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT wilaya ya Ukerewe amemshukuru Mbunge huyo wa Viti Maalum huku akimuahidi ushirikiano katika kuleta maendeleo kwa jamii na kuimarisha chama.
Ziara hiyo ya Uimarishaji wa chama na jumuiya yake, Utekelezaji wa shughuli za maendeleo na utatuzi wa kero za wananchi pia iliambata na Kikao Cha kawaida cha Baraza la UWT wilaya, ilihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo hilo, Kaimu Katibu wa UWT Mkoa wa Mwanza na baadhi ya wajumbe wa Baraza la UWT Mkoa.
















No comments:
Post a Comment